Nehemiah 11:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, viongozi wa watu wakakaa mjini Yerusalemu; watu wengine wote, wakapiga kura kati ya kila jamaa kumi ili kuchagua jamaa moja itakayokaa mjini Yerusalemu, mji mtakatifu. Jamaa nyingine tisa zikakaa katika miji yao mingine.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi viongozi wa watu walikaa Yerusalemu, nao watu wale wengine walipiga kura ili kuleta mtu mmoja kati ya watu kumi aje kuishi Yerusalemu, mji mtakatifu, nao wengine tisa waliobaki wakae katika miji yao wenyewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, wakuu wa watu walikuwa wakikaa Yerusalemu; nao watu waliosalia wakapiga kura, ili katika watu kumi kumleta mmoja akae ndani ya Yerusalemu mji mtakatifu, na wale kenda wakae mijini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, viongozi wa watu wakakaa mjini Yerusalemu; watu wengine wote, wakapiga kura kati ya kila jamaa kumi ili kuchagua jamaa moja itakayokaa mjini Yerusalemu, mji mtakatifu. Jamaa nyingine tisa zikakaa katika miji yao mingine.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi, viongozi wa watu waliokaa Yerusalemu na watu wengine, walipiga kura mtu mmoja kati ya watu kumi aje kuishi Yerusalemu, mji mtakatifu, wengine tisa waliobaki ilikuwa wakae katika miji yao wenyewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi viongozi wa watu walikaa Yerusalemu, nao watu wale wengine walipiga kura ili kuleta mtu mmoja kati ya watu kumi aje kuishi Yerusalemu, mji mtakatifu, nao wengine tisa waliobaki wakae katika miji yao wenyewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, viongozi wa watu walikuwa wakikaa Yerusalemu; nao watu waliosalia wakapiga kura, ili katika watu kumi kumleta mmoja akae ndani ya Yerusalemu mji mtakatifu, na wale tisa wakae mijini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, viongozi wa watu wakakaa mjini Yerusalemu; watu wengine wote, wakapiga kura kati ya kila jamaa kumi ili kuchagua jamaa moja itakayokaa mjini Yerusalemu, mji mtakatifu. Jamaa nyingine tisa zikakaa katika miji yao mingine.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakuu wa watu wakaja kukaa Yerusalemu, lakini watu wengine wakapiga kura, katika kila watu kumi wapate mmoja wa kumpeleka kukaa Yerusalemu ulio mji mtakatifu; wale wengine tisa wakae mijini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, wakuu wa watu walikuwa wakikaa Yerusalemu; nao watu waliosalia wakapiga kura, ili katika watu kumi kumleta mmoja akae ndani ya Yerusalemu mji mtakatifu, na wale kenda wakae mijini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, viongozi wa watu wakakaa katika Yerusalema; watu wengine wote, wakapiga kura kati ya kila jamaa kumi kwa kuchagua jamaa moja itakayokaa katika Yerusalema, muji mutakatifu. Jamaa zingine tisa zikakaa katika miji yao mingine.