Nehemiah 11:30 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Zanoa na Adulamu pamoja na vijiji vilivyoizunguka, Lakishi na mashamba yaliyouzunguka, na katika Azeka pamoja na vijiji vilivyouzunguka. Hii ina maana kwamba watu wa Yuda walikaa katika eneo lililoko kati ya Beer-sheba upande wa kusini na Bonde la Hinomu upande wa kaskazini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zanoa, Adulamu na vijiji vyake, katika Lakishi na mashamba yake, na katika Azeka na makazi yake. Hivyo walikuwa wakiishi kuanzia Beer-Sheba hadi Bonde la Hinomu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Zanoa, Adulamu na vijiji vyake, Lakishi na mashamba yake, Azeka na vijiji vyake. Hivyo wakatua toka Beer-sheba mpaka bonde la Hinomu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Zanoa na Adulamu pamoja na vijiji vilivyoizunguka, Lakishi na mashamba yaliyouzunguka, na katika Azeka pamoja na vijiji vilivyouzunguka. Hii ina maana kwamba watu wa Yuda walikaa katika eneo lililoko kati ya Beer-sheba upande wa kusini na Bonde la Hinomu upande wa kaskazini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zanoa, Adulamu na vijiji vyazo, katika Lakishi na mashamba yake, katika Azeka na makazi yake. Hivyo walikuwa wakiishi kuanzia Beer-Sheba mpaka Bonde la Hinomu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zanoa, Adulamu na vijiji vyake, katika Lakishi na mashamba yake, na katika Azeka na makazi yake. Hivyo walikuwa wakiishi kuanzia Beer-Sheba mpaka Bonde la Hinomu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Zanoa, Adulamu na vijiji vyake, Lakishi na mashamba yake, Azeka na vijiji vyake. Hivyo wakakaa toka Beer-sheba mpaka bonde la Hinomu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Zanoa na Adulamu pamoja na vijiji vilivyoizunguka, Lakishi na mashamba yaliyouzunguka, na katika Azeka pamoja na vijiji vilivyouzunguka. Hii ina maana kwamba watu wa Yuda walikaa katika eneo lililoko kati ya Beer-sheba upande wa kusini na Bonde la Hinomu upande wa kaskazini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Zanoa, Adulamu na katika viwanja vyao. Lakisi na mashambani kwake, Azeka na katika vijiji vyake; basi, wakatua toka Beri-Seba hata bonde la Hinomu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Zanoa, Adulamu na vijiji vyake, Lakishi na mashamba yake, Azeka na vijiji vyake. Hivyo wakatua toka Beer-sheba mpaka bonde la Hinomu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Zanoa na Adulamu pamoja na vijiji vilivyoizunguka, Lakisi na mashamba yanayouzunguka, na katika Azeka pamoja na vijiji vinavyouzunguka. Hii ina maana kwamba watu wa Yuda walikaa katika eneo linalokuwa kati ya Beri-Seba upande wa kusini na Bonde la Hinomu upande wa Kaskazini.