Nehemiah 12:31 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Niliwakusanya viongozi wote wa Yuda kwenye ukuta na kutenga waimbaji katika makundi mawili makubwa yaliyoimba nyimbo za shukrani wakiwa katika maandamano. Kundi moja lilielekea upande wa kulia wa ukuta hadi kwenye Lango la Takataka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Niliwaagiza viongozi wa Yuda wapande juu ya ukuta. Pia niliagiza makundi mawili makubwa ya waimbaji waimbe nyimbo za kumshukuru Mungu. Kundi moja lilipanda juu ya ukuta upande wa kuume, kuelekea Lango la Samadi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo nikawapandisha wakuu wa Yuda juu ya ukuta, nikawaagiza mikutano mikubwa miwili ya hao walioshukuru, na kuandamana; mmoja uende kwa kuume ukutani kuliendea lango la jaa;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Niliwakusanya viongozi wote wa Yuda kwenye ukuta na kutenga waimbaji katika makundi mawili makubwa yaliyoimba nyimbo za shukrani wakiwa katika maandamano. Kundi moja lilielekea upande wa kulia wa ukuta hadi kwenye Lango la Takataka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Niliwaagiza viongozi wa Yuda wapande juu ya ukuta. Pia niliagiza makundi mawili makubwa ya waimbaji waimbe nyimbo za kumshukuru Mungu. Moja lipande juu ya ukuta upande wa kuume, kuelekea Lango la Samadi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Niliwaagiza viongozi wa Yuda wapande juu ya ukuta. Pia niliagiza makundi mawili makubwa ya waimbaji waimbe nyimbo za kumshukuru Mungu. Kundi moja lilipanda juu ya ukuta upande wa kuume, kuelekea Lango la Samadi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo nikawapandisha viongozi wa Yuda juu ya ukuta, nikawatenga makundi mawili makubwa ya hao walioandamana na kushukuru, liende upande wa kulia ukutani kuliendea lango la jaa;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Niliwakusanya viongozi wote wa Yuda kwenye ukuta na kutenga waimbaji katika makundi mawili makubwa yaliyoimba nyimbo za shukrani wakiwa katika maandamano. Kundi moja lilielekea upande wa kulia wa ukuta hadi kwenye Lango la Takataka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha nikawapeleka wakuu wa Yuda bomani juu, nikasimama hapo na makundi mawili makubwa ya kushukuru, moja likaenda ukutani juu kufika penye lango la Jaani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo nikawapandisha wakuu wa Yuda juu ya ukuta, nikawaagiza mikutano mikubwa miwili ya hao walioshukuru, na kuandamana; mmoja uende kwa kuume ukutani kuliendea lango la jaa;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nikawakusanya viongozi wote wa Yuda kwenye ukuta na kutenga waimbaji katika makundi mawili makubwa yaliyoimba nyimbo za shukrani wakiwa katika maandamano. Kundi moja lilielekea upande wa kuume wa ukuta mpaka kwenye Mulango wa Takataka.