Nehemiah 13:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wengine toka mji wa Tiro walileta samaki na bidhaa nyingine mjini Yerusalemu na kuwauzia watu wetu siku ya Sabato.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu kutoka Tiro walioishi Yerusalemu walileta samaki na aina nyingi za bidhaa na kuziuza Yerusalemu siku ya Sabato kwa watu wa Yuda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena wakakaa humo watu wa Tiro, walioleta samaki, na biashara za kila namna, wakawauzia wana wa Yuda siku ya sabato, na mumo humo Yerusalemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wengine toka mji wa Tiro walileta samaki na bidhaa nyingine mjini Yerusalemu na kuwauzia watu wetu siku ya Sabato.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu kutoka Tiro waliokuwa wakiishi Yerusalemu walileta samaki na aina nyingi za bidhaa na kuziuza Yerusalemu siku ya Sabato kwa watu wa Yuda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu kutoka Tiro waliokuwa wakiishi Yerusalemu walileta samaki na aina nyingi za bidhaa na kuziuza Yerusalemu siku ya Sabato kwa watu wa Yuda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena watu wa Tiro walioleta samaki na biashara za kila namna wakakaa mumo humo, wakawauzia watu wa Yuda na Yerusalemu siku ya sabato.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wengine toka mji wa Tiro walileta samaki na bidhaa nyingine mjini Yerusalemu na kuwauzia watu wetu siku ya Sabato.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao Watiro waliokaa huku wakaleta samaki na vingine vyo vyote vya kuuza, wakaviuzia wana wa Yuda namo mle Yerusalemu siku ya mapumziko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena wakakaa humo watu wa Tiro, walioleta samaki, na biashara za kila namna, wakawauzia wana wa Yuda siku ya sabato, na mumo humo Yerusalemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wengine toka muji wa Tiro walileta samaki na biashara nyingine Yerusalema na kuwauzishia watu wetu siku ya Sabato.