Nehemiah 13:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, babu zetu hawakufanya uovu wa namna hii hii na kumfanya Mungu wetu kutuletea maafa pamoja na mji huu? Na bado mnaleta ghadhabu yake juu ya watu wa Israeli kwa kuikufuru Sabato.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, baba zenu hawakufanya mambo kama haya, hata wakamsababisha Mungu wetu kuleta maafa haya yote juu yetu na juu ya mji huu? Sasa bado mnazidi kuchochea ghadhabu yake dhidi ya Israeli kwa kuinajisi Sabato.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Sivyo hivyo walivyofanya baba zenu; na Mungu wetu, je! Hakuyaleta mabaya haya yote juu yetu, na juu ya mji huu? Nanyi hata hivyo mwazidi kuleta ghadhabu juu ya Israeli kwa kuinajisi sabato!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, babu zetu hawakufanya uovu wa namna hii hii na kumfanya Mungu wetu kutuletea maafa pamoja na mji huu? Na bado mnaleta ghadhabu yake juu ya watu wa Israeli kwa kuikufuru Sabato.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, baba zenu hawakufanya mambo ya jinsi hii hata kumsababisha Mungu wetu kuleta maafa haya yote juu yetu na juu ya mji huu? Sasa bado mnazidi kuchochea ghadhabu yake dhidi ya Israeli kwa kuinajisi Sabato.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, baba zenu hawakufanya mambo kama haya, hata wakamsababisha Mungu wetu kuleta maafa haya yote juu yetu na juu ya mji huu? Sasa bado mnazidi kuchochea ghadhabu yake dhidi ya Israeli kwa kuinajisi Sabato.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Sivyo hivyo walivyofanya baba zenu; na Mungu wetu, je! Hakuyaleta mabaya haya yote juu yetu, na juu ya mji huu? Nanyi hata hivyo mnazidi kuleta ghadhabu juu ya Israeli kwa kuinajisi sabato!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, babu zetu hawakufanya uovu wa namna hii hii na kumfanya Mungu wetu kutuletea maafa pamoja na mji huu? Na bado mnaleta ghadhabu yake juu ya watu wa Israeli kwa kuikufuru Sabato.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Je? Baba zenu hawakuyafanya yayo hayo? Hii siyo sababu, Mungu wetu akituletea haya mabaya sisi na mji huu? Kumbe ninyi mwataka kuwapatia Waisiraeli makali yenye moto yaliyo makubwa zaidi, mkiichafua siku ya mapumziko!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Sivyo hivyo walivyofanya baba zenu; na Mungu wetu, je! Hakuyaleta mabaya haya yote juu yetu, na juu ya mji huu? Nanyi hata hivyo mwazidi kuleta ghadhabu juu ya Israeli kwa kuinajisi sabato!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Babu zetu hawakufanya uovu wa namna hiihii na kumusukuma Mungu wetu kutuletea hasara pamoja na muji huu? Na munazidi kuamusha kasirani yake juu ya watu wa Israeli kwa kuchafua siku ya Sabato.”