Nehemiah 13:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Niliwakemea na kuwaapiza, hata nikawapiga baadhi yao na kuwavuta nywele zao. Niliwalazimisha kuapa kwa jina la Mungu, nikisema, “Binti zenu msiwaoze kwa vijana wao, wala binti zao wasiolewe na vijana wenu au na nyinyi wenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Niliwakemea na kuwalaani. Niliwapiga baadhi ya watu na kung’oa nywele zao. Niliwaapisha kwa jina la Mungu na kusema: “Msiwaoze binti zenu kwa wana wao, wala binti zao wasiolewe na wana wenu wala ninyi wenyewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikagombana nao, nikawalaani, nikawapiga baadhi yao, na kuwang'oa nywele zao; nikawaapisha kwa Mungu, nikasema, Msiwaoze wana wao binti zenu, wala msiwatwae binti zao ili waolewe na wana wenu, wala na ninyi wenyewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Niliwakemea na kuwaapiza, hata nikawapiga baadhi yao na kuwavuta nywele zao. Niliwalazimisha kuapa kwa jina la Mungu, nikisema, “Binti zenu msiwaoze kwa vijana wao, wala binti zao wasiolewe na vijana wenu au na nyinyi wenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Niliwakemea na kuwalaani. Niliwapiga baadhi ya watu na kung'oa nywele zao. Niliwaapisha kwa jina la Mungu na kusema: “Msiwaoze binti zenu kwa wana wao, wala binti zao wasiolewe na wana wenu wala ninyi wenyewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Niliwakemea na kuwalaani. Niliwapiga baadhi ya watu na kung’oa nywele zao. Niliwaapisha kwa jina la Mungu na kusema: “Msiwaoze binti zenu kwa wana wao, wala binti zao wasiolewe na wana wenu wala ninyi wenyewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikagombana nao, nikawalaani, nikawapiga baadhi yao, na kuwang'oa nywele zao; nikawaapisha kwa Mungu, nikasema, Msiwaoze wana wao binti zenu, wala msiwatwae binti zao ili waolewe na wana wenu, wala na ninyi wenyewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Niliwakemea na kuwaapiza, hata nikawapiga baadhi yao na kuwavuta nywele zao. Niliwalazimisha kuapa kwa jina la Mungu, nikisema, “Binti zenu msiwaoze kwa vijana wao, wala binti zao wasiolewe na vijana wenu au na nyinyi wenyewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikawagombeza na kuwaapiza na kuwapiga, waume wengine nikawavuta nywele. Kisha nikawaapisha na kumtaja Mungu kwamba: Msiwaoze wana wao wana wenu wa kike, wala msichukue kwao wana wa kike, mwape wana wenu wa kiume au mwaoe wenyewe!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikagombana nao, nikawalaani, nikawapiga baadhi yao, na kuwang’oa nywele zao; nikawaapisha kwa Mungu, nikasema, Msiwaoze wana wao binti zenu, wala msiwatwae binti zao ili waolewe na wana wenu, wala na ninyi wenyewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nikawakaripia na kuwalaani, hata nikawapiga wamoja kati yao na kuwaongoa nywele zao. Nikawalazimisha kuapa kwa jina la Mungu, nikisema: “Wabinti zenu musiwaoeshe kwa vijana wao, wala wabinti zao wasiolewe na vijana wenu au na ninyi wenyewe.