Nehemiah 13:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, Solomoni hakutenda dhambi kwa sababu ya wanawake wa namna hiyo? Yeye alikuwa mfalme mkuu kuliko wafalme wa mataifa mengine. Mungu alimpenda na akamfanya kuwa mfalme juu ya watu wote wa Israeli, hata hivyo wanawake wa mataifa mengine, walimfanya hata yeye atende dhambi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, Sulemani hakutenda dhambi kwa sababu ya wanawake wa aina hiyo? Miongoni mwa mataifa mengi hapakuwa na mfalme kama yeye. Alipendwa na Mungu wake. Naye Mungu alimweka kuwa mfalme juu ya Israeli yote, lakini hata yeye, wanawake wa mataifa mengine walimfanya atende dhambi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Sulemani, mwana wa Daudi, hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengi hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. Tena alipendwa na Mungu wake, naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli; walakini wanawake wageni walimkosesha hata yeye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, Solomoni hakutenda dhambi kwa sababu ya wanawake wa namna hiyo? Yeye alikuwa mfalme mkuu kuliko wafalme wa mataifa mengine. Mungu alimpenda na akamfanya kuwa mfalme juu ya watu wote wa Israeli, hata hivyo wanawake wa mataifa mengine, walimfanya hata yeye atende dhambi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, Solomoni hakutenda dhambi kwa sababu ya wanawake wa namna hiyo? Miongoni mwa mataifa mengi hapakuwepo mfalme kama yeye. Alipendwa na Mungu wake. Naye Mungu alimweka kuwa mfalme juu ya Israeli yote, hata hivyo wanawake wa mataifa mengine walimfanya hata yeye atende dhambi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, Sulemani hakutenda dhambi kwa sababu ya wanawake wa namna hiyo? Miongoni mwa mataifa mengi hapakuwepo mfalme kama yeye. Alipendwa na Mungu wake. Naye Mungu alimweka kuwa mfalme juu ya Israeli yote, lakini hata yeye, wanawake wa mataifa mengine walimfanya atende dhambi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Sulemani, mwana wa Daudi, hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengi hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. Tena alipendwa na Mungu wake, naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli; lakini wanawake wageni walimkosesha hata yeye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, Solomoni hakutenda dhambi kwa sababu ya wanawake wa namna hiyo? Yeye alikuwa mfalme mkuu kuliko wafalme wa mataifa mengine. Mungu alimpenda na akamfanya kuwa mfalme juu ya watu wote wa Israeli, hata hivyo wanawake wa mataifa mengine, walimfanya hata yeye atende dhambi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Je? Siyo haya, Salomo, mfalme wa Isiraeli, aliyoyakosa? Katika mataifa mengi hakuwako mfalme kama yeye, naye alikuwa amependwa na Mungu wake, kwa hiyo Mungu akampa kuwa mfalme wa Waisiraeli wote; lakini naye yeye wanawake wageni wakamkosesha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Sulemani, mwana wa Daudi, hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengi hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. Tena alipendwa na Mungu wake, naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli; walakini wanawake wageni walimkosesha hata yeye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Si Solomono alitenda zambi kwa sababu ya wanawake wa namna hiyo? Yeye alikuwa mufalme mukubwa kuliko wafalme wa mataifa mengine. Mungu akamupenda na akamufanya kuwa mufalme juu ya watu wote wa Israeli, hata hivyo wanawake wa mataifa mengine, wakamusukuma kutenda zambi.