Nehemiah 13:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati mambo haya yalipokuwa yanatendeka mimi sikuwako Yerusalemu; kwani katika mwaka wa thelathini na mbili wa utawala wa mfalme Artashasta wa Babuloni, nilikuwa nimeomba likizo; nami nikaenda kutoa ripoti kwake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini wakati haya yote yalipokuwa yakitendeka, sikuwa Yerusalemu, kwa kuwa katika mwaka wa thelathini na mbili wa utawala wa Artashasta mfalme wa Babeli nilikuwa nimerudi kwa mfalme. Baadaye nilimwomba ruhusa,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini wakati huo wote mimi sikuwako huko Yerusalemu; maana katika mwaka wa thelathini na mbili wa Artashasta, mfalme wa Babeli, nalimrudia mfalme; na baada ya siku kadha wa kadha nikaomba ruhusa tena kwa mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati mambo haya yalipokuwa yanatendeka mimi sikuwako Yerusalemu; kwani katika mwaka wa thelathini na mbili wa utawala wa mfalme Artashasta wa Babuloni, nilikuwa nimeomba likizo; nami nikaenda kutoa ripoti kwake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini wakati haya yote yalipokuwa yakitendeka, sikuwa Yerusalemu, kwa kuwa katika mwaka wa thelathini na mbili wa kutawala Artashasta mfalme wa Babeli nilikuwa nimerudi kwa mfalme. Baadaye nilimwomba ruhusa,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini wakati haya yote yalipokuwa yakitendeka, sikuwa Yerusalemu, kwa kuwa katika mwaka wa thelathini na mbili wa utawala wa Artashasta mfalme wa Babeli nilikuwa nimerudi kwa mfalme. Baadaye nilimwomba ruhusa,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini wakati huo wote mimi sikuwako huko Yerusalemu; maana katika mwaka wa thelathini na mbili wa Artashasta, mfalme wa Babeli, nilimrudia mfalme; na baada ya siku kadhaa nikaomba ruhusa tena kwa mfalme.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati mambo haya yalipokuwa yanatendeka mimi sikuwako Yerusalemu; kwani katika mwaka wa thelathini na mbili wa utawala wa mfalme Artashasta wa Babuloni, nilikuwa nimeomba likizo; nami nikaenda kutoa ripoti kwake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hayo yote yalipofanyika, mimi nilikuwa simo Yerusalemu, kwani katika mwaka wa thelathini na mbili wa Artasasta, mfalme wa Babeli, nalikwenda kwake mfalme; siku zilipopita, nikamwomba mfalme ruhusa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini wakati huo wote mimi sikuwako huko Yerusalemu; maana katika mwaka wa thelathini na mbili wa Artashasta, mfalme wa Babeli, nalimrudia mfalme; na baada ya siku kadha wa kadha nikaomba ruhusa tena kwa mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati mambo haya yalipokuwa yanatendeka mimi sikukuwa Yerusalema; maana katika mwaka wa makumi tatu na mbili wa utawala wa mufalme Artasasta wa Babeli, nilikuwa nimeomba ruhusa; nami nikaenda kwake.