Nehemiah 2:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika mwezi wa Nisani, katika mwaka wa ishirini wa utawala wa mfalme Artashasta, wakati divai ilipokuwa mbele yake, nilichukua divai na kumpelekea mkononi mwake. Kamwe sikuwahi kuwa mwenye huzuni mbele yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika mwezi wa Nisani, mwaka wa ishirini wa utawala wa Mfalme Artashasta, wakati divai ilipoletwa kwake, niliichukua na kumpa mfalme. Sikuwahi kuonekana mwenye huzuni mbele yake kabla ya hapo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa katika mwezi wa Nisani, mwaka wa ishirini wa mfalme Artashasta, na divai imewekwa mbele yake, nikaishika ile divai, nikampa mfalme. Nami mpaka sasa sikuwa na huzuni mbele ya mfalme wakati wo wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika mwezi wa Nisani, katika mwaka wa ishirini wa utawala wa mfalme Artashasta, wakati divai ilipokuwa mbele yake, nilichukua divai na kumpelekea mkononi mwake. Kamwe sikuwahi kuwa mwenye huzuni mbele yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika mwezi wa Nisani mwaka wa ishirini wa kutawala kwake Mfalme Artashasta, wakati divai ilipoletwa kwa ajili yake, niliichukua na kumpa mfalme. Sikuwahi kuonekana mwenye huzuni mbele yake kabla ya hapo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika mwezi wa Nisani mwaka wa ishirini wa utawala wa Mfalme Artashasta, wakati divai ilipoletwa kwake, niliichukua na kumpa mfalme. Sikuwahi kuonekana mwenye huzuni mbele yake kabla ya hapo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa katika mwezi wa Nisani, mwaka wa ishirini wa mfalme Artashasta, na divai imewekwa mbele yake, nikaishika ile divai, nikampa mfalme. Nami mpaka sasa sikuwa na huzuni mbele ya mfalme wakati wowote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika mwezi wa Nisani, katika mwaka wa ishirini wa utawala wa mfalme Artashasta, wakati divai ilipokuwa mbele yake, nilichukua divai na kumpelekea mkononi mwake. Kamwe sikuwahi kuwa mwenye huzuni mbele yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa katika mwezi wa Nisani wa mwaka wa ishirini wa mfalme Artasasta; hapo, mvinyo ilipowekwa mbele yake, nikaichukua hiyo mvinyo, nikampa mfalme; lakini mpaka hapo sijawa nikinuna mbele yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa katika mwezi wa Nisani, mwaka wa ishirini wa mfalme Artashasta, na divai imewekwa mbele yake, nikaishika ile divai, nikampa mfalme. Nami mpaka sasa sikuwa na huzuni mbele ya mfalme wakati wo wote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika mwezi wa Nisani, kwa mwaka wa makumi mbili wa utawala wa mufalme Artasasta, wakati divai ilipokuwa mbele yake, nilitwaa divai na kumupatia mufalme. Mpaka sasa nilikuwa sijapata kuwa na huzuni mbele yake.