Nehemiah 2:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nikatoka nikipitia Lango la Bondeni katika njia ielekeayo kwenye Kisima cha Joka na Lango la Mavi; nikazikagua kuta za mji wa Yerusalemu ambazo zilikuwa zimebomolewa pamoja na malango yake ambayo yalikuwa yameteketezwa kwa moto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nikatoka nje usiku kupitia Lango la Bondeni, kuelekea Kisima cha Joka na Lango la Samadi, nikikagua kuta za Yerusalemu zilizokuwa zimebomolewa, na malango yake yaliyokuwa yameteketezwa kwa moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikatoka nje usiku, kwa njia ya lango la bondeni, nikashika njia iendayo kisima cha joka, na lango la jaa; nikazitazama kuta za Yerusalemu, zilizokuwa zimebomoka; na malango yake yameteketezwa kwa moto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nikatoka nikipitia Lango la Bondeni katika njia ielekeayo kwenye Kisima cha Joka na Lango la Mavi; nikazikagua kuta za mji wa Yerusalemu ambazo zilikuwa zimebomolewa pamoja na malango yake ambayo yalikuwa yameteketezwa kwa moto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nikatoka nje usiku kupitia Lango la Bondeni, kuelekea Kisima cha Joka na Lango la Samadi, nikikagua kuta za Yerusalemu, zilizokuwa zimebomolewa na malango yake yaliyokuwa yameteketezwa kwa moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nikatoka nje usiku kupitia Lango la Bondeni, kuelekea Kisima cha Joka na Lango la Samadi, nikikagua kuta za Yerusalemu zilizokuwa zimebomolewa, na malango yake yaliyokuwa yameteketezwa kwa moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikatoka nje usiku, kwa njia ya lango la bondeni, nikashika njia iendayo kwenye kisima cha joka, na lango la jaa; nikazitazama kuta za Yerusalemu, zilizokuwa zimebomoka; na malango yake yameteketezwa kwa moto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nikatoka nikipitia Lango la Bondeni katika njia ielekeayo kwenye Kisima cha Joka na Lango la Mavi; nikazikagua kuta za mji wa Yerusalemu ambazo zilikuwa zimebomolewa pamoja na malango yake ambayo yalikuwa yameteketezwa kwa moto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikatoka usiku huo katika lango la Bondeni, nikashika njia ya kwenda penye kisima cha Joka na penye lango la Jaani, nikawa nikizichungulia kuta za Yerusalemu zilizokuwa zimebomolewa, nayo malango yaliyokuwa yameliwa na moto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikatoka nje usiku, kwa njia ya lango la bondeni, nikashika njia iendayo kisima cha joka, na lango la jaa; nikazitazama kuta za Yerusalemu, zilizokuwa zimebomoka; na malango yake yameteketezwa kwa moto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nikatoka nikipitia kwenye Mulango wa Bonde katika njia inayoelekea kwenye Kisima cha Joka na mulango wa Yalala; nikachunguza kuta za muji wa Yerusalema ambazo zilikuwa zimebomolewa pamoja na milango yake ambayo ilikuwa imeteketezwa kwa moto.