Nehemiah 2:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maofisa hawakujua mahali nilipokuwa nimekwenda wala nimefanya nini. Tena nilikuwa sijawaambia Wayahudi, makuhani, viongozi, wakuu wala wale watu ambao wangeifanya kazi ya kuujenga upya mji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Maafisa hawakujua nilikoenda wala nilichokuwa nikifanya, kwa sababu nilikuwa bado sijasema lolote kwa Wayahudi, wala makuhani, wala wakuu, wala maafisa, wala mtu yeyote ambaye angefanya kazi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala mashehe hawakujua nilikokwenda, wala nilivyotenda; wala sijawaambia Wayahudi, wala makuhani, wala wakuu, wala mashehe, wala watu wengine waliokuwa wakiifanya kazi hiyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maofisa hawakujua mahali nilipokuwa nimekwenda wala nimefanya nini. Tena nilikuwa sijawaambia Wayahudi, makuhani, viongozi, wakuu wala wale watu ambao wangeifanya kazi ya kuujenga upya mji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Maafisa hawakujua nilikokwenda wala nilichokuwa nikifanya, kwa sababu mpaka sasa nilikuwa bado sijasema lo lote kwa Wayahudi wala makuhani wala wakuu wala maafisa wala mtu ye yote ambaye angefanya kazi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Maafisa hawakujua nilikokwenda wala nilichokuwa nikifanya, kwa sababu mpaka sasa nilikuwa bado sijasema lolote kwa Wayahudi, wala makuhani, wala wakuu, wala maafisa, wala mtu yeyote ambaye angefanya kazi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala maofisa hawakujua nilikokwenda, wala niliyotenda; tena nilikuwa sijawaambia Wayahudi, makuhani, wakuu, maofisa, wala watu wengine waliokuwa wakiifanya kazi hiyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maofisa hawakujua mahali nilipokuwa nimekwenda wala nimefanya nini. Tena nilikuwa sijawaambia Wayahudi, makuhani, viongozi, wakuu wala wale watu ambao wangeifanya kazi ya kuujenga upya mji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wakuu hawakujua, wala nilikokwenda, wala niliyoyafanya; nami mpaka hapo sikuwaambia Wayuda neno lo lote, wala watambikaji, wala wakuu wa mji, wala watawalaji, wala wao wengine, niliowatakia kazi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala mashehe hawakujua nilikokwenda, wala nilivyotenda; wala sijawaambia Wayahudi, wala makuhani, wala wakuu, wala mashehe, wala watu wengine waliokuwa wakiifanya kazi hiyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakubwa hawakujua pahali nilipokuwa nimekwenda wala nimefanya nini. Tena nilikuwa sijawaambia Wayuda, makuhani, viongozi, wakubwa wala wale watu ambao wangefanya kazi ya kujenga upya muji.