Nehemiah 2:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nikawaeleza jinsi Mungu alivyokuwa pamoja nami akinitendea kwa wema wake. Nikawaeleza pia maneno ambayo mfalme alikuwa ameniambia. Wao walipoyasikia hayo, wakasema, “Haya, na tuanze kazi ya ujenzi.” Hivyo wakajiandaa kwa kazi hiyo njema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia niliwaambia kuhusu mkono wenye neema wa Mungu wangu uliokuwa juu yangu, na kile mfalme alichokuwa ameniambia. Wakajibu, “Haya! Tuanze kujenga tena.” Kwa hiyo wakaanza kazi hii njema.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikawaeleza habari ya mkono wa Mungu wangu ulivyokuwa mwema juu yangu; pia na maneno ya mfalme aliyoniambia. Nao wakasema, Haya! Na tuondoke tukajenge. Basi wakaitia mikono yao nguvu kwa kazi hiyo njema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nikawaeleza jinsi Mungu alivyokuwa pamoja nami akinitendea kwa wema wake. Nikawaeleza pia maneno ambayo mfalme alikuwa ameniambia. Wao walipoyasikia hayo, wakasema, “Haya, na tuanze kazi ya ujenzi.” Hivyo wakajiandaa kwa kazi hiyo njema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia niliwaambia kuhusu mkono wenye neema wa Mungu wangu uliokuwa juu yangu na kile mfalme alichokuwa ameniambia. Wakajibu, “Haya na tuanze kujenga tena.” Kwa hiyo wakaanza kazi hii njema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia niliwaambia kuhusu mkono wenye neema wa Mungu wangu uliokuwa juu yangu, na kile mfalme alichokuwa ameniambia. Wakajibu, “Haya! Tuanze kujenga tena.” Kwa hiyo wakaanza kazi hii njema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikawaeleza habari ya mkono wa Mungu wangu ulivyokuwa mwema juu yangu; pia na maneno ya mfalme aliyoniambia. Nao wakasema, Haya! Na tuondoke tukajenge. Basi wakaitia mikono yao nguvu kwa kazi hiyo njema.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nikawaeleza jinsi Mungu alivyokuwa pamoja nami akinitendea kwa wema wake. Nikawaeleza pia maneno ambayo mfalme alikuwa ameniambia. Wao walipoyasikia hayo, wakasema, “Haya, na tuanze kazi ya ujenzi.” Hivyo wakajiandaa kwa kazi hiyo njema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikawasimulia, mkono wa Mungu ulio mwema ulivyonisaidia, nayo yale maneno, mfalme aliyoniambia. Ndipo, walipoitikia kwamba: Na tuinuke, tujenge! Nayo mikono yao wakaishupaza kufanya kazi njema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikawaeleza habari ya mkono wa Mungu wangu ulivyokuwa mwema juu yangu; pia na maneno ya mfalme aliyoniambia. Nao wakasema, Haya! Na tuondoke tukajenge. Basi wakaitia mikono yao nguvu kwa kazi hiyo njema.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nikawaelezea jinsi Mungu alivyokuwa pamoja nami akinitendea kwa wema wake. Nikawaelezea vilevile maneno ambayo mufalme alikuwa ameniambia. Wao waliposikia hayo, wakasema: “Sasa, na tuanze kazi ya ujenzi.” Hivyo wakajitayarisha kwa kazi hiyo njema.