Nehemiah 2:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nikawajibu, “Mungu wa mbinguni atatufanikisha katika kazi hii, nasi tulio watumishi wake tutaanza ujenzi. Lakini nyinyi hamna fungu wala haki wala kumbukumbu katika mji wa Yerusalemu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nikawajibu kwa kusema, “Mungu wa mbinguni atatufanikisha. Sisi watumishi wake tutaanza kujenga upya, lakini ninyi hamna sehemu wala dai lolote, wala kumbukumbu la haki katika Yerusalemu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo nikawajibu, nikawaambia, Mungu wa mbinguni, yeye atatufanikisha; kwa hiyo sisi, watumishi wake, tutaondoka na kujenga; lakini ninyi hamna sehemu, wala haki, wala kumbukumbu, katika Yerusalemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nikawajibu, “Mungu wa mbinguni atatufanikisha katika kazi hii, nasi tulio watumishi wake tutaanza ujenzi. Lakini nyinyi hamna fungu wala haki wala kumbukumbu katika mji wa Yerusalemu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nikawajibu kwa kusema, “Mungu wa mbinguni atatufanikisha. Sisi watumishi wake tutaanza kujenga upya, lakini kwenu ninyi, hamna sehemu wala dai lo lote wala kumbukumbu la haki katika Yerusalemu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nikawajibu kwa kusema, “Mungu wa mbinguni atatufanikisha. Sisi watumishi wake tutaanza kujenga upya, lakini kwenu ninyi, hamna sehemu wala dai lolote wala kumbukumbu la haki katika Yerusalemu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo nikawajibu, nikawaambia, Mungu wa mbinguni, yeye atatufanikisha; kwa hiyo sisi, watumishi wake, tutaondoka na kujenga; lakini ninyi hamna sehemu, wala haki, wala kumbukumbu, katika Yerusalemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nikawajibu, “Mungu wa mbinguni atatufanikisha katika kazi hii, nasi tulio watumishi wake tutaanza ujenzi. Lakini nyinyi hamna fungu wala haki wala kumbukumbu katika mji wa Yerusalemu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikawajibu neno nikiwaambia: Mungu wa mbinguni atatupa kuimaliza kazi hii; sisi tulio watumwa wake tutainuka, tujenge. Lakini ninyi hamna fungu humu Yerusalemu wala cho chote kilicho chenu wala ukumbusho tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo nikawajibu, nikawaambia, Mungu wa mbinguni, yeye atatufanikisha; kwa hiyo sisi, watumishi wake, tutaondoka na kujenga; lakini ninyi hamna sehemu, wala haki, wala kumbukumbu, katika Yerusalemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nikawajibu: “Mungu wa mbinguni atatufanikisha katika kazi hii, nasi tunaokuwa watumishi wake tutaanza kujenga. Lakini ninyi hamuna sehemu au haki wala ukumbusho katika Yerusalema.”