Nehemiah 2:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Halafu nikamwambia mfalme, “Ee mfalme, ikiwa unapendezwa nami na ikiwa nimepata upendeleo mbele yako, nakuomba unitume Yuda ili niende kuujenga upya mji ambamo yamo makaburi ya babu zangu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
na nikamjibu mfalme, “Ikimpendeza mfalme, na kama mtumishi wako amepata kibali machoni pake, anitume kule mji wa Yuda, mahali baba zangu walipozikwa, ili niweze kuujenga upya.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikamwambia mfalme, Mfalme akiona vema, na ikiwa mimi, mtumishi wako, nimepata kibali machoni pako, tafadhali unipeleke mpaka Yuda, niuendee mji wa makaburi ya baba zangu, nipate kuujenga.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Halafu nikamwambia mfalme, “Ee mfalme, ikiwa unapendezwa nami na ikiwa nimepata upendeleo mbele yako, nakuomba unitume Yuda ili niende kuujenga upya mji ambamo yamo makaburi ya babu zangu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
nikamjibu mfalme, “Kama ikimpendeza mfalme na kama mtumishi wako amepata kibali machoni pake na anitume Yuda kwenye mji mahali baba zangu walipozikwa ili niweze kuujenga upya.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
na nikamjibu mfalme, “Kama ikimpendeza mfalme, na kama mtumishi wako amepata kibali machoni pake, anitume kule mji wa Yuda, mahali baba zangu walipozikwa, ili niweze kuujenga upya.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikamwambia mfalme, Mfalme akiona vema, na ikiwa mimi, mtumishi wako, nimepata kibali machoni pako, tafadhali unitume mpaka Yuda, niende katika mji wa makaburi ya baba zangu, nipate kuujenga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Halafu nikamwambia mfalme, “Ee mfalme, ikiwa unapendezwa nami na ikiwa nimepata upendeleo mbele yako, nakuomba unitume Yuda ili niende kuujenga upya mji ambamo yamo makaburi ya babu zangu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nikamwambia mfalme: Vikiwa vema machoni pako, mfalme, mtumwa wako naye akiwa mwema machoni pako, nitume, niende katika nchi ya Yuda mle mjini mlimo na makaburi ya baba zangu, miujenge!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikamwambia mfalme, Mfalme akiona vema, na ikiwa mimi, mtumishi wako, nimepata kibali machoni pako, tafadhali unipeleke mpaka Yuda, niuendee mji wa makaburi ya baba zangu, nipate kuujenga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu nikamwambia mufalme: “Ee mufalme, ikikupendeza na ikiwa nimepata kukubaliwa mbele yako, ninakuomba unitume katika inchi ya Yuda kusudi niende kuujenga upya muji ambamo muko makaburi ya babu zangu.”