Nehemiah 2:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nikamjibu, “Ee mfalme ikiwa unapendezwa nami, naomba nipewe barua ili nizipeleke kwa watawala wa mkoa wa magharibi ya mto Eufrate ili waniruhusu nipite hadi nchini Yuda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia nikamwambia, “Ikimpendeza mfalme, naomba nipewe barua kwa watawala wa Ng’ambo ya Frati, ili wanipe ulinzi hadi nifike Yuda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena nikamwambia mfalme, Mfalme akiona vema, na nipewe nyaraka kwa maliwali walio ng'ambo ya Mto, ili waniache kupita mpaka nifike Yuda;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nikamjibu, “Ee mfalme ikiwa unapendezwa nami, naomba nipewe barua ili nizipeleke kwa watawala wa mkoa wa magharibi ya mto Eufrate ili waniruhusu nipite hadi nchini Yuda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia nikamwambia, “Kama ikimpendeza mfalme, naomba nipewe barua kwa watawala wa Ng'ambo ya Eufrati, ili wanipe ulinzi mpaka nifike Yuda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia nikamwambia, “Kama ikimpendeza mfalme, naomba nipewe barua kwa watawala wa Ng’ambo ya Frati, ili wanipe ulinzi mpaka nifike Yuda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena nikamwambia mfalme, Mfalme akiona vema, na nipewe nyaraka kwa watawala walio ng'ambo ya Mto, ili wanikubalie kupita hadi nifike Yuda;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nikamjibu, “Ee mfalme ikiwa unapendezwa nami, naomba nipewe barua ili nizipeleke kwa watawala wa mkoa wa magharibi ya mto Eufrate ili waniruhusu nipite hadi nchini Yuda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha nikamwambia mfalme: Vikiwa vema kwake mfalme, na wanipe barua za kuwapelekea wenye amri walioko ng'ambo ya huko ya jito kubwa, waniache, nipite, mpaka nitakapofika Yuda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena nikamwambia mfalme, Mfalme akiona vema, na nipewe nyaraka kwa maliwali walio ng’ambo ya Mto, ili waniache kupita mpaka nifike Yuda;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nikamujibu: “Ee mufalme, ikikupendeza, ninaomba nipewe barua kusudi nizipeleke kwa watawala wa jimbo la upande wa magaribi wa muto Furati kusudi waniruhusu nipite mpaka katika inchi ya Yuda.