Nehemiah 2:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilipowafikia wakuu wa mkoa wa magharibi ya mto Eufrate, niliwapa barua za mfalme. Mfalme alikuwa amenituma pamoja na maofisa wa jeshi na wapandafarasi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi nilienda kwa watawala wa Ng’ambo ya Frati na kuwapa barua za mfalme. Pia mfalme alikuwa ametuma maafisa wa jeshi na askari wapanda farasi pamoja nami.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo nikafika kwa maliwali walio ng'ambo ya Mto, nikawapa hizo nyaraka za mfalme. Naye mfalme alikuwa amepeleka maakida wa jeshi lake na wapanda farasi pamoja nami.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilipowafikia wakuu wa mkoa wa magharibi ya mto Eufrate, niliwapa barua za mfalme. Mfalme alikuwa amenituma pamoja na maofisa wa jeshi na wapandafarasi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi nilikwenda kwa watawala wa Ng'ambo ya Eufrati na kuwapa barua za mfalme. Pia mfalme alikuwa ametuma maafisa wa jeshi na askari wapanda farasi pamoja nami.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi nilienda kwa watawala wa Ng’ambo ya Frati na kuwapa barua za mfalme. Pia mfalme alikuwa ametuma maafisa wa jeshi na askari wapanda farasi pamoja nami.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo nikafika kwa watawala wa mkoa walio ng'ambo ya Mto, nikawapa nyaraka hizo za mfalme. Naye mfalme alikuwa ametuma maofisa wa jeshi lake na wapanda farasi pamoja nami.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilipowafikia wakuu wa mkoa wa magharibi ya mto Eufrate, niliwapa barua za mfalme. Mfalme alikuwa amenituma pamoja na maofisa wa jeshi na wapandafarasi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nilipofika kwao wenye amri ng'ambo ya huku ya jito kubwa, nikawapa zile barua za mfalme. Tena mfalme alikuwa amenipa hata wakuu wenye vikosi vya askari nao wapanda farasi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo nikafika kwa maliwali walio ng’ambo ya Mto, nikawapa hizo nyaraka za mfalme. Naye mfalme alikuwa amepeleka maakida wa jeshi lake na wapanda farasi pamoja nami.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilipowafikia wakubwa wa jimbo la upande wa magaribi wa muto Furati, nikawapa barua za mufalme. Mufalme alikuwa amenituma pamoja na wakubwa wa waaskari na waaskari wapanda-farasi.