Nehemiah 3:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi Lango la Kondoo lilijengwa upya na Eliashibu, kuhani mkuu, pamoja na ndugu zake waliokuwa makuhani. Waliliweka wakfu na kutia milango yake; wakaliweka wakfu tangu Mnara wa Mia Moja hadi Mnara wa Hananeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Eliashibu kuhani mkuu na makuhani wenzake walienda kufanya kazi na kulijenga upya Lango la Kondoo. Waliliweka wakfu na kuweka milango mahali pake, wakajenga hadi kufikia Mnara wa Mia, ambao waliuweka wakfu hadi Mnara wa Hananeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo akaondoka Eliashibu, kuhani mkuu, pamoja na nduguze makuhani, wakalijenga lango la kondoo; wakazitia boriti zake, wakaisimamisha milango yake; mpaka mnara wa Hamea wakalitakasa, mpaka mnara wa Hananeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi Lango la Kondoo lilijengwa upya na Eliashibu, kuhani mkuu, pamoja na ndugu zake waliokuwa makuhani. Waliliweka wakfu na kutia milango yake; wakaliweka wakfu tangu Mnara wa Mia Moja hadi Mnara wa Hananeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Eliyashibu Kuhani Mkuu na makuhani wenzake walikwenda kufanya kazi na kulijenga upya Lango la Kondoo. Waliliweka wakfu na kuweka milango mahali pake, wakajenga hadi kufikia Mnara wa Mia Moja, ambao waliuweka wakfu hadi Mnara wa Hananeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Eliashibu kuhani mkuu na makuhani wenzake walikwenda kufanya kazi na kulijenga upya Lango la Kondoo. Waliliweka wakfu na kuweka milango mahali pake, wakajenga hadi kufikia Mnara wa Mia, ambao waliuweka wakfu hadi Mnara wa Hananeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo akaondoka Eliashibu, kuhani mkuu, pamoja na nduguze makuhani, wakalijenga lango la kondoo; wakazitia boriti zake, wakaisimamisha milango yake; mpaka mnara wa Hamea wakalitakasa, mpaka mnara wa Hananeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi Lango la Kondoo lilijengwa upya na Eliashibu, kuhani mkuu, pamoja na ndugu zake waliokuwa makuhani. Waliliweka wakfu na kutia milango yake; wakaliweka wakfu tangu Mnara wa Mia Moja hadi Mnara wa Hananeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, alipoondokea mtambikaji mkuu Eliasibu pamoja na ndugu zake waliokuwa watambikaji, wakalijenga lango la Kondoo. Kisha wakalieua, wakaitia milango yake, kisha wakajenga kufikia penye mnara wa Hamea, wakaueua, wakaendelea kujenga kufikia penye mnara wa Hananeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo akaondoka Eliashibu, kuhani mkuu, pamoja na nduguze makuhani, wakalijenga lango la kondoo; wakazitia boriti zake, wakaisimamisha milango yake; mpaka mnara wa Hamea wakalitakasa, mpaka mnara wa Hananeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi Eliasubu, Kuhani Mukubwa, pamoja na wandugu zake waliokuwa makuhani wakasimama na kuanza kujenga Mulango wa kondoo. Wakautakasa na kutia milango yake; wakaitakasa tangia kwenye Munara wa Mia Moja mpaka Munara wa Hananeli.