Nehemiah 3:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sehemu inayofuata ilijengwa upya na Shalumu, mwana wa Haloheshi, mtawala wa nusu nyingine ya wilaya ya Yerusalemu. Alisaidiana na binti zake katika ujenzi huo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Shalumu mwana wa Haloheshi, mtawala wa nusu ya wilaya ya Yerusalemu, alikarabati sehemu iliyofuatia akisaidiwa na binti zake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na baada yake akafanyiza Shalumu, mwana wa Haloheshi, akida wa nusu ya Yerusalemu, yeye na binti zake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sehemu inayofuata ilijengwa upya na Shalumu, mwana wa Haloheshi, mtawala wa nusu nyingine ya wilaya ya Yerusalemu. Alisaidiana na binti zake katika ujenzi huo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Shalumu mwana wa Haloheshi, mtawala wa nusu ya wilaya ya Yerusalemu, alikarabati sehemu iliyofuatia akisaidiana na binti zake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Shalumu mwana wa Haloheshi, mtawala wa nusu ya wilaya ya Yerusalemu, alikarabati sehemu iliyofuatia akisaidiwa na binti zake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na baada yake akajenga Shalumu, mwana wa Haloheshi, mtawala wa nusu ya sehemu ya Yerusalemu, yeye na binti zake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sehemu inayofuata ilijengwa upya na Shalumu, mwana wa Haloheshi, mtawala wa nusu nyingine ya wilaya ya Yerusalemu. Alisaidiana na binti zake katika ujenzi huo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kando yake akafanya kazi Salumu, mwana wa Halohesi, aliyekuwa mkuu wa nusu ya pili ya mtaa wa Yerusalemu, yeye na wanawe wa kike.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na baada yake akafanyiza Shalumu, mwana wa Haloheshi, akida wa nusu ya Yerusalemu, yeye na binti zake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sehemu inayofuata ikajengwa upya na Salumu mwana wa Halohesi, mutawala wa nusu nyingine ya wilaya ya Yerusalema. Alisaidiana na binti zake katika ujenzi huo.