Nehemiah 3:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lango la Bondeni lilijengwa upya na Hanuni pamoja na wakazi wa mji wa Zanoa. Wakayaweka malango mahali pake, wakatia bawaba na makomeo yake. Waliujenga upya ukuta ukiwa na urefu wa mita 400 hivi hadi Lango la Samadi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lango la Bondeni lilikarabatiwa na Hanuni na wakazi wa Zanoa. Walilijenga upya, na kuweka milango yake na makomeo na nondo mahali pake. Pia walikarabati ukuta wenye urefu wa dhiraa elfu moja hadi Lango la Samadi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lango la bondeni wakalifanyiza Hanuni, nao wakaao Zanoa; wakalijenga, wakaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake, na huo ukuta wa dhiraa elfu mpaka lango la jaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lango la Bondeni lilijengwa upya na Hanuni pamoja na wakazi wa mji wa Zanoa. Wakayaweka malango mahali pake, wakatia bawaba na makomeo yake. Waliujenga upya ukuta ukiwa na urefu wa mita 400 hivi hadi Lango la Samadi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lango la Bondeni lilikarabatiwa na Hanuni na wakazi wa Zanoa. Walilijenga kwa upya na kuweka milango yake na makomeo na nondo mahali pake. Pia walikarabati ukuta wenye urefu wa mita 450 hadi Lango la Samadi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lango la Bondeni lilikarabatiwa na Hanuni na wakazi wa Zanoa. Walilijenga upya, na kuweka milango yake na makomeo na nondo mahali pake. Pia walikarabati ukuta wenye urefu wa mita 450 hadi Lango la Samadi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lango la bondeni wakalijenga Hanuni, nao wakaao Zanoa; wakalijenga, wakaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake, na huo ukuta wa dhiraa elfu moja mpaka lango la jaa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lango la Bondeni lilijengwa upya na Hanuni pamoja na wakazi wa mji wa Zanoa. Wakayaweka malango mahali pake, wakatia bawaba na makomeo yake. Waliujenga upya ukuta ukiwa na urefu wa mita 400 hivi hadi Lango la Samadi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lango la Bondeni wakalitengeneza Hanuni na wenyeji wa Zanoa; walipokwisha kulijenga, wakaitia milango yake na makomeo yake na miti yake ya kukingia, kisha wakatengeneza mikono elfu ya boma mpaka lango la Jaani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lango la bondeni wakalifanyiza Hanuni, nao wakaao Zanoa; wakalijenga, wakaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake, na huo ukuta wa dhiraa elfu mpaka lango la jaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mulango wa Bonde ukajengwa upya na Hanuni pamoja na wakaaji wa muji wa Zanoa. Wakaweka milango pahali pake, wakatia vyuma na vifungio vyake. Wakajenga upya ukuta ukiwa na urefu wa metre mia ine hivi mpaka kwenye mulango wa Yalala.