Nehemiah 3:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lango la Samadi lilijengwa upya na Malkiya, mwana wa Rekabu, mkuu wa wilaya ya Beth-hakeremu. Akaliweka lango mahali pake, akatia bawaba na makomeo yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lango la Samadi lilikarabatiwa na Malkiya mwana wa Rekabu, mtawala wa wilaya ya Beth-Hakeremu. Alilijenga upya, na kuweka milango yake, na makomeo na nondo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na lango la jaa akalifanyiza Malkiya, mwana wa Rekabu, akida wa mtaa wa Beth-hakeremu; akalijenga, akaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lango la Samadi lilijengwa upya na Malkiya, mwana wa Rekabu, mkuu wa wilaya ya Beth-hakeremu. Akaliweka lango mahali pake, akatia bawaba na makomeo yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lango la Samadi lilikarabatiwa na Malkiya mwana wa Rekabu, mtawala wa wilaya ya Beth-Hakeremu. Alijenga kwa upya na kuweka milango yake makomeo na nondo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lango la Samadi lilikarabatiwa na Malkiya mwana wa Rekabu, mtawala wa wilaya ya Beth-Hakeremu. Alilijenga upya, na kuweka milango yake, na makomeo na nondo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na lango la jaa akalijenga Malkiya, mwana wa Rekabu, mtawala wa sehemu ya wa Beth-hakeremu; akalijenga, akaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lango la Samadi lilijengwa upya na Malkiya, mwana wa Rekabu, mkuu wa wilaya ya Beth-hakeremu. Akaliweka lango mahali pake, akatia bawaba na makomeo yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lango la Jaani akalitengeneza Malkia, mwana wa Rekabu, aliyekuwa mkuu wa mtaa wa Beti-Keremu, alipokwisha kulijenga, akalitia milango yake na makomeo yake na miti yake ya kukingia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na lango la jaa akalifanyiza Malkiya, mwana wa Rekabu, akida wa mtaa wa Beth-hakeremu; akalijenga, akaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mulango wa Yalala ukajengwa upya na Malkiya mwana wa Rekabu, mukubwa wa wilaya ya Beti-Hakeremu. Akaweka mulango kwa nafasi yake, akatia vyuma na vifungio vyake.