Nehemiah 3:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lango la Chemchemi lilijengwa upya na Shalumu, mwana wa Kolhoze, mkuu wa wilaya ya Mizpa. Akalifunika, akaliweka lango mahali pake, akatia bawabu na makomeo yake. Kwenye Bwawa la Shela akajenga ukuta ulio karibu na bustani ya kifalme hadi ngazi zinazoshuka toka mji wa mfalme Daudi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lango la Chemchemi lilikarabatiwa na Shalumu mwana wa Kolhoze, mtawala wa wilaya ya Mispa. Alilijenga upya, akaliezeka na kuweka milango yake, na makomeo na nondo mahali pake. Pia alikarabati ukuta wa Bwawa la Siloamu karibu na Bustani ya Mfalme, hadi kwenye ngazi zinazoshuka kutoka Mji wa Daudi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na lango la chemchemi akalifanyiza Shalumu, mwana wa Kolhoze, akida wa mtaa wa Mispa; akalijenga na kulifunika, akaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake, na huo ukuu wa birika la Shiloa karibu na bustani ya mfalme, mpaka madaraja yashukayo kutoka mji wa Daudi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lango la Chemchemi lilijengwa upya na Shalumu, mwana wa Kolhoze, mkuu wa wilaya ya Mizpa. Akalifunika, akaliweka lango mahali pake, akatia bawabu na makomeo yake. Kwenye Bwawa la Shela akajenga ukuta ulio karibu na bustani ya kifalme hadi ngazi zinazoshuka toka mji wa mfalme Daudi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lango la Chemchemi lilikarabatiwa na Shalumu mwana wa Kolhoze, mtawala wa wilaya ya Mispa. Alilijenga kwa upya, akaliezeka na kuweka milango yake, makomeo yake na nondo mahali pake. Pia alikarabati ukuta wa Bwawa la Siloamu karibu na Bustani ya Mfalme hadi kwenye ngazi zinazoshuka kutoka Mji wa Daudi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lango la Chemchemi lilikarabatiwa na Shalumu mwana wa Kolhoze, mtawala wa wilaya ya Mispa. Alilijenga upya, akaliezeka na kuweka milango yake, na makomeo na nondo mahali pake. Pia alikarabati ukuta wa Bwawa la Siloamu karibu na Bustani ya Mfalme, hadi kwenye ngazi zinazoshuka kutoka Mji wa Daudi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na lango la chemchemi akalijenga Shalumu, mwana wa Kolhoze, mkuu wa Mispa akalitengeneza lango la Chemchemi akalijenga na kulifunika, akasimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake, na huo ukuu wa birika la Shiloa karibu na bustani ya mfalme, mpaka madaraja yashukayo kutoka mji wa Daudi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lango la Chemchemi lilijengwa upya na Shalumu, mwana wa Kolhoze, mkuu wa wilaya ya Mizpa. Akalifunika, akaliweka lango mahali pake, akatia bawabu na makomeo yake. Kwenye Bwawa la Shela akajenga ukuta ulio karibu na bustani ya kifalme hadi ngazi zinazoshuka toka mji wa mfalme Daudi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lango la Jicho la Maji akalitengeneza Saluni, mwana wa Koli-Hoze, aliyekuwa mkuu wa mtaa wa Misipa; alipokwisha kulijenga na kulifunika juu, akaitia milango yake na makomeo yake na miti yake ya kukingia; kisha akaujenga ukuta penye ziwa la Sela karibu ya bustani ya mfalme mpaka penye ngazi inayoshuka toka mjini kwa Dawidi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na lango la chemchemi akalifanyiza Shalumu, mwana wa Kolhoze, akida wa mtaa wa Mispa; akalijenga na kulifunika, akaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake, na huo ukuu wa birika la Shiloa karibu na bustani ya mfalme, mpaka madaraja yashukayo kutoka mji wa Daudi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mulango wa Chemichemi ukajengwa upya na Salumu mwana wa Koli-Hoze, mukubwa wa wilaya ya Misipa. Akaufunika, akauweka mulango kwa nafasi yake, akatia vyuma na vifungio vyake. Kwenye Kisima cha Sela akajenga ukuta unaokuwa karibu na bustani ya kifalme mpaka kwenye ngazi zinazoshuka toka muji wa mufalme Daudi.