Nehemiah 3:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sehemu inayofuata hadi kwenye makaburi ya Daudi, bwawa na majengo ya jeshi ilijengwa upya na Nehemia, mwana wa Azbuki, mkuu wa nusu ya wilaya ya Beth-suri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada yake, Nehemia mwana wa Azbuki, mtawala wa nusu ya wilaya ya Beth-Suri, alikarabati kufikia mkabala na makaburi ya Daudi, hadi kwenye bwawa lililotengenezwa, na kufikia Nyumba ya Mashujaa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Baada yake akafanyiza Nehemia, mwana wa Azbuki, akida wa nusu ya mtaa wa Beth-suri, mpaka mahali paelekeapo makaburi ya Daudi, na mpaka birika lililofanyizwa, na mpaka nyumba ya mashujaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sehemu inayofuata hadi kwenye makaburi ya Daudi, bwawa na majengo ya jeshi ilijengwa upya na Nehemia, mwana wa Azbuki, mkuu wa nusu ya wilaya ya Beth-suri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sehemu iliyofuatia, Nehemia mwana wa Azbuki, mtawala wa nusu ya wilaya ya Beth-Zuri, alikarabati kufikia mkabala na makaburi ya Daudi, mpaka kwenye bwawa lililotengenezwa na kufikia Nyumba ya Mashujaa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada yake, Nehemia mwana wa Azbuki, mtawala wa nusu ya wilaya ya Beth-Suri, alikarabati kufikia mkabala na makaburi ya Daudi, mpaka kwenye bwawa lililotengenezwa, na kufikia Nyumba ya Mashujaa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Baada yake akajenga Nehemia, mwana wa Azbuki, mkuu wa nusu ya mtaa wa Beth-suri, mpaka mahali paelekeapo makaburi ya Daudi, na mpaka birika lililofanyizwa, na mpaka nyumba ya wapiganaji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sehemu inayofuata hadi kwenye makaburi ya Daudi, bwawa na majengo ya jeshi ilijengwa upya na Nehemia, mwana wa Azbuki, mkuu wa nusu ya wilaya ya Beth-suri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nyuma yake akafanya kazi Nehemia, mwana wa Azibuku, aliyekuwa mkuu wa nusu ya mtaa wa Beti-Suri mpaka hapo panapoyaelekea makaburi ya Dawidi penye lile ziwa lililotengenezwa hapo, tena mpaka nyumba ya mafundi wa vita.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Baada yake akafanyiza Nehemia, mwana wa Azbuki, akida wa nusu ya mtaa wa Beth-suri, mpaka mahali paelekeapo makaburi ya Daudi, na mpaka birika lililofanyizwa, na mpaka nyumba ya mashujaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sehemu inayofuata mpaka kwenye makaburi ya Daudi, kisima na majengo ya waaskari ikajengwa upya na Nehemia mwana wa Aibuki, mukubwa wa nusu ya wilaya ya Beti-Suri.