Nehemiah 3:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sehemu inayofuata inayoelekeana na ghala ya silaha kwenye pembe ya ukuta ilijengwa upya na Ezeri, mwana wa Yeshua, mkuu wa Mizpa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada yao, Ezeri mwana wa Yeshua, mtawala wa Mispa, alikarabati sehemu nyingine, kuanzia ile sehemu inayotazamana na mwinuko wa kuelekea kwenye ghala la kuhifadhia silaha, hadi kwenye pembe ya ukuta.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na baada yake akafanyiza Ezeri, mwana wa Yeshua, akida wa Mispa, sehemu nyingine, kupaelekea penye kupanda kwa ghala ya silaha, ukuta ugeukapo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sehemu inayofuata inayoelekeana na ghala ya silaha kwenye pembe ya ukuta ilijengwa upya na Ezeri, mwana wa Yeshua, mkuu wa Mizpa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sehemu iliofuatia, Ezeri mwana wa Yeshua, mtawala wa Mispa, alikarabati sehemu nyingine, kuanzia ile sehemu inayotazamana na mwinuko wa kuelekea kwenye ghala la kuhifadhia silaha, mpaka kwenye pembe ya ukuta.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada yao, Ezeri mwana wa Yeshua, mtawala wa Mispa, alikarabati sehemu nyingine, kuanzia ile sehemu inayotazamana na mwinuko wa kuelekea kwenye ghala la kuhifadhia silaha, mpaka kwenye pembe ya ukuta.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na baada yake Ezeri, mwana wa Yeshua, mkuu wa Mispa, akajenga sehemu nyingine, inayoelekeana na njia ya kupanda kwa ghala ya silaha, pembeni mwa ukuta.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sehemu inayofuata inayoelekeana na ghala ya silaha kwenye pembe ya ukuta ilijengwa upya na Ezeri, mwana wa Yeshua, mkuu wa Mizpa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kando yake akafanya kazi Ezeri, mwana wa Yesua, aliyekuwa mkuu wa Misipa, akatengeneza kipande kingine kielekeacho pa kupandia penye nyumba ya mata huko pembeni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na baada yake akafanyiza Ezeri, mwana wa Yeshua, akida wa Mispa, sehemu nyingine, kupaelekea penye kupanda kwa ghala ya silaha, ukuta ugeukapo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sehemu inayofuata inayoelekeana na gala ya silaha kwenye pembe ya ukuta ikajengwa upya na Ezeri mwana wa Yesua, mutawala wa Misipa.