Nehemiah 3:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sehemu inayofuata tangu pembeni hadi kwenye mlango wa Eliashibu, kuhani mkuu, ilijengwa upya na Baruku, mwana wa Zabai.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada yake, Baruku mwana wa Zakai alikarabati kwa bidii sehemu nyingine kuanzia ile pembe, hadi kwenye lango la nyumba ya Eliashibu kuhani mkuu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Baada yake Baruki, mwana wa Zakai, akafanyiza kwa bidii sehemu nyingine, toka ugeukapo ukuta mpaka mlango wa nyumba ya Eliashibu, kuhani mkuu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sehemu inayofuata tangu pembeni hadi kwenye mlango wa Eliashibu, kuhani mkuu, ilijengwa upya na Baruku, mwana wa Zabai.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sehemu iliofuatia, Baruki mwana wa Zabai alikarabati kwa bidii sehemu nyingine kuanzia ile pembe mpaka kwenye lango la nyumba ya Eliyashibu Kuhani Mkuu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada yake, Baruku mwana wa Zakai alikarabati kwa bidii sehemu nyingine kuanzia ile pembe, mpaka kwenye lango la nyumba ya Eliashibu kuhani mkuu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Baada yake Baruku, mwana wa Zakai, akajenga kwa bidii sehemu nyingine, kutoka pembeni mwa ukuta mpaka mlango wa nyumba ya Eliashibu, kuhani mkuu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sehemu inayofuata tangu pembeni hadi kwenye mlango wa Eliashibu, kuhani mkuu, ilijengwa upya na Baruku, mwana wa Zabai.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nyuma yake akafanya kazi na kujihimiza Baruku, mwana wa Zabai, akatengeneza kipande kingine kutoka hapo pembeni kufikia mlango wa nyumba ya mtambikaji mkuu Eliasibu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Baada yake Baruki, mwana wa Zakai, akafanyiza kwa bidii sehemu nyingine, toka ugeukapo ukuta mpaka mlango wa nyumba ya Eliashibu, kuhani mkuu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sehemu inayofuata tangia kwenye pembe mpaka kwenye mulango wa Eliasibu, Kuhani Mukubwa, ikajengwa upya na Baruku mwana wa Zabayi.