Nehemiah 3:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sehemu inayofuata tangu mlangoni mwa nyumba ya Eliashibu, kuhani mkuu, hadi mwisho wa nyumba hiyo, ilijengwa upya na Meremothi, mwana wa Uria, mwana wa Hakosi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kupakana naye, Meremothi mwana wa Uria, mwana wa Hakosi, alikarabati sehemu nyingine, kuanzia penye lango la nyumba ya Eliashibu hadi mwisho wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Baada yake akafanyiza Meremothi, mwana wa Uria, mwana wa Hakosi, sehemu nyingine, toka mlango wa nyumba ya Eliashibu mpaka mwisho wa nyumba ya Eliashibu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sehemu inayofuata tangu mlangoni mwa nyumba ya Eliashibu, kuhani mkuu, hadi mwisho wa nyumba hiyo, ilijengwa upya na Meremothi, mwana wa Uria, mwana wa Hakosi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sehemu iliofuatia, Meremothi mwana wa Uria, mwana wa Hakosi, alikarabati sehemu nyingine, kuanzia penye lango la nyumba ya Eliyashibu mpaka mwisho wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kupakana naye, Meremothi mwana wa Uria, mwana wa Hakosi, alikarabati sehemu nyingine, kuanzia penye lango la nyumba ya Eliashibu mpaka mwisho wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Baada yake akajenga Meremothi, mwana wa Uria, mwana wa Hakosi, sehemu nyingine, kutoka mlangoni mwa nyumba ya Eliashibu mpaka mwisho wa nyumba ya Eliashibu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sehemu inayofuata tangu mlangoni mwa nyumba ya Eliashibu, kuhani mkuu, hadi mwisho wa nyumba hiyo, ilijengwa upya na Meremothi, mwana wa Uria, mwana wa Hakosi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nyuma yake akafanya kazi Meremoti, mwana wa Uria, mwana wa Hakosi, akatengeneza kipande kingine kutoka mlango wa nyumba ya Eliasibu kufikia mwisho wa nyumba ya Eliasibu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Baada yake akafanyiza Meremothi, mwana wa Uria, mwana wa Hakosi, sehemu nyingine, toka mlango wa nyumba ya Eliashibu mpaka mwisho wa nyumba ya Eliashibu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sehemu inayofuata tangia kwenye mulango wa nyumba ya Eliasibu, Kuhani Mukubwa, mpaka mwisho wa nyumba hiyo, ikajengwa upya na Meremoti mwana wa Uria, mujukuu wa Hakosi.