Nehemiah 3:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sehemu inayofuata, ilijengwa upya na Uzieli, mwana wa Harkaya, mfua dhahabu. Sehemu inayofuata hadi Ukuta Mpana ilijengwa upya na Hanania, mtengenezaji wa marashi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Uzieli mwana wa Harhaya, mmoja wa masonara, alikarabati sehemu iliyofuatia, naye Hanania mmoja wa watengenezaji marashi akakarabati sehemu iliyofuatia. Walitengeneza Yerusalemu kufikia Ukuta Mpana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na baada yao akafanyiza Uzieli, mwana wa Harhaya, mmoja wa mafundi wa dhahabu. Na baada yake akafanyiza Hanania, mmoja wa mafundi wa manukato, nao wakaujengea Yerusalemu buruji mpaka ule ukuta mpana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sehemu inayofuata, ilijengwa upya na Uzieli, mwana wa Harkaya, mfua dhahabu. Sehemu inayofuata hadi Ukuta Mpana ilijengwa upya na Hanania, mtengenezaji wa marashi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Uzieli mwana wa Harhaya, mmoja wa masonara, walikarabati sehemu iliyofuatia na Hanania mmoja wa watengenezaji marashi, alikarabati sehemu iliyofuatia. Walitengeneza Yerusalemu mpaka kufikia Ukuta Mpana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Uzieli mwana wa Harhaya, mmoja wa masonara, alikarabati sehemu iliyofuatia, naye Hanania mmoja wa watengenezaji marashi akakarabati sehemu iliyofuatia. Walitengeneza Yerusalemu mpaka kufikia Ukuta Mpana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na baada yao akajenga Uzieli, mwana wa Harhaya, mmoja wa mafundi wa dhahabu. Na baada yake akafanyiza Hanania, mmoja wa mafundi wa manukato, nao wakaujengea Yerusalemu buruji mpaka ule ukuta mpana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sehemu inayofuata, ilijengwa upya na Uzieli, mwana wa Harkaya, mfua dhahabu. Sehemu inayofuata hadi Ukuta Mpana ilijengwa upya na Hanania, mtengenezaji wa marashi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kando yao wakafanya kazi Uzieli, mwana wa Harihaya, pamoja na wafua dhahabu; kando yake akafanya kazi Hanania, mwana wa chama cha watengeneza manukato; nao wakaujenga Yerusalemu mpaka penye Ukuta Mpana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na baada yao akafanyiza Uzieli, mwana wa Harhaya, mmoja wa mafundi wa dhahabu. Na baada yake akafanyiza Hanania, mmoja wa mafundi wa manukato, nao wakaujengea Yerusalemu buruji mpaka ule ukuta mpana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sehemu inayofuata, ilijengwa upya na Usieli mwana wa Harihaya, mufua zahabu. Sehemu inayofuata mpaka kwenye Ukuta Mupana ikajengwa upya na Hanania, mutengenezaji wa marasi.