Nehemiah 4:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wayahudi waliokaa miongoni mwa adui zetu waliposikia maneno yao, walitujia mara kumi wakisema, “Watakuja toka kila mahali wanapokaa na kutushambulia.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Wayahudi ambao waliishi karibu nao walikuja zaidi ya mara kumi na kutuambia, “Popote mtakapoelekea, watatushambulia.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha ikawa, Wayahudi walipokuja, wale waliokaa karibu nao, wakatuambia mara kumi, Kutoka kila mahali mtakaporejea watatushambulia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wayahudi waliokaa miongoni mwa adui zetu waliposikia maneno yao, walitujia mara kumi wakisema, “Watakuja toka kila mahali wanapokaa na kutushambulia.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Wayahudi ambao waliishi karibu nao walikuja zaidi ya mara kumi na kutuambia, “Po pote mtakapoelekea, watatushambulia.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Wayahudi ambao waliishi karibu nao walikuja zaidi ya mara kumi na kutuambia, “Popote mtakapoelekea, watatushambulia.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Wayahudi waliokaa karibu nao, walikuja, wakatuambia mara kumi: Watakuja kutoka kila sehemu wanapokaa kutushambulia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wayahudi waliokaa miongoni mwa adui zetu waliposikia maneno yao, walitujia mara kumi wakisema, “Watakuja toka kila mahali wanapokaa na kutushambulia.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Wayuda waliokaa kandokando yao walipotuambia hata mara kumi wakitoka po pote vijijini mwao: Sharti mrudi kwetu,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha ikawa, Wayahudi walipokuja, wale waliokaa karibu nao, wakatuambia mara kumi, Kutoka kila mahali mtakaporejea watatushambulia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila mujengaji alikuwa na upanga wake ukifungwa kwenye kiuno chake naye akiendelea kujenga. Na mutu wa kupiga baragumu alikuwa karibu nami.