Nehemiah 4:19 — Compare Translations
10 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nikawaambia wakuu, maofisa na watu wote kwa ujumla “Kazi ni kubwa, nayo imeenea sehemu kubwa hivi ya kwamba tumetawanyika mno juu ya ukuta kila mmoja yuko mbali na mwenzake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha nikawaambia wakuu, maafisa na watu wengine wote, “Kazi hii ni kubwa na imeenea sehemu kubwa, nasi tumetawanyika kila mmoja akiwa mbali na mwenzake katika ukuta.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikawaambia wakuu, na mashehe na watu wengine; Kazi hii ni nyingi, tena kubwa, nasi tumetawanyika juu ya ukuta, kila mtu mbali na mwenzake;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nikawaambia wakuu, maofisa na watu wote kwa ujumla “Kazi ni kubwa, nayo imeenea sehemu kubwa hivi ya kwamba tumetawanyika mno juu ya ukuta kila mmoja yuko mbali na mwenzake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha nikawaambia wakuu, maafisa na watu wengine wote, “Kazi hii ni kubwa na imeenea sehemu kubwa, nasi tumetawanyika kila mmoja yuko mbali na mwenzake juu ya ukuta.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha nikawaambia wakuu, maafisa na watu wengine wote, “Kazi hii ni kubwa na imeenea sehemu kubwa, nasi tumetawanyika kila mmoja akiwa mbali na mwenzake juu ya ukuta.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikawaambia wakuu, maofisa na watu wengine; Kazi hii ni nyingi, tena kubwa, nasi tumetawanyika juu ya ukuta, kila mtu akiwa mbali na mwenzake;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nikawaambia wakuu, maofisa na watu wote kwa ujumla “Kazi ni kubwa, nayo imeenea sehemu kubwa hivi ya kwamba tumetawanyika mno juu ya ukuta kila mmoja yuko mbali na mwenzake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikawaambia wakuu wa miji na watawalaji na watu wengine wote pia: Hapa, tunapofanyia kazi zetu za kujenga, ni parefu mno, nasi tuko tumetawanyika ukutani, tunasimama mbali kidogo, kila mtu na mwenziwe;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikawaambia wakuu, na mashehe na watu wengine; Kazi hii ni nyingi, tena kubwa, nasi tumetawanyika juu ya ukuta, kila mtu mbali na mwenzake;