Nehemiah 4:21 — Compare Translations

10 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo, tukaendelea kufanya kazi yetu na nusu ya watu wakishika silaha tangu mapambazuko hadi nyota zinapoonekana mbinguni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi tuliendelea na kazi, nusu ya watu wakishikilia mikuki, kuanzia mawio ya jua hadi nyota zilipoonekana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hivyo tukajitia katika kazi hiyo; na nusu yao waliishika mikuki, tangu alfajiri hata nyota zikatokea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo, tukaendelea kufanya kazi yetu na nusu ya watu wakishika silaha tangu mapambazuko hadi nyota zinapoonekana mbinguni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi tuliendelea na kazi, nusu ya watu wakishikilia mikuki, kuanzia maawio ya jua hadi nyota zilipoonekana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi tuliendelea na kazi, nusu ya watu wakishikilia mikuki, kuanzia mawio ya jua hadi nyota zilipoonekana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hivyo tukajitia katika kazi hiyo; na nusu yao waliishika mikuki, tangu alfajiri hadi nyota zikatokea.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo, tukaendelea kufanya kazi yetu na nusu ya watu wakishika silaha tangu mapambazuko hadi nyota zinapoonekana mbinguni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, tulivyozifanya kazi zetu, nusu yao wakishika mikuki tangu hapo, jua lilipokucha, hata nyota zilipotokea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hivyo tukajitia katika kazi hiyo; na nusu yao waliishika mikuki, tangu alfajiri hata nyota zikatokea.