Nehemiah 4:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini tuliendelea na ujenzi wa ukuta mpaka ukafikia nusu yake kwa sababu watu walikuwa wamedhamiria kwa dhati.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi tuliujenga upya ukuta hadi wote ukafikia nusu ya kimo chake, kwa kuwa watu walifanya kazi kwa moyo wote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi tukaujenga ukuta; nao ukuta wote ukaungamanishwa kiasi cha nusu ya kimo chake; maana watu walikuwa na moyo wa kufanya kazi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini tuliendelea na ujenzi wa ukuta mpaka ukafikia nusu yake kwa sababu watu walikuwa wamedhamiria kwa dhati.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi tuliujenga upya ukuta mpaka wote ukafikia nusu ya kimo chake, kwa kuwa watu walifanya kazi kwa moyo wote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi tuliujenga upya ukuta mpaka wote ukafikia nusu ya kimo chake, kwa kuwa watu walifanya kazi kwa moyo wote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi tukaujenga ukuta; nao ukuta wote ukaunganishwa kiasi cha nusu ya kimo chake; maana watu walikuwa na moyo wa kufanya kazi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini tuliendelea na ujenzi wa ukuta mpaka ukafikia nusu yake kwa sababu watu walikuwa wamedhamiria kwa dhati.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, tukalijenga boma; kuta zote za boma zilipopandishwa na kufika katikati ya urefu wa juu, watu wakajikaza kujenga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi tukaujenga ukuta; nao ukuta wote ukaungamanishwa kiasi cha nusu ya kimo chake; maana watu walikuwa na moyo wa kufanya kazi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wayuda waliokaa kati ya waadui zetu waliposikia maneno yao, mara kwa mara, walitufikia mara kumi wakisema: “Watakuja toka kila pahali wanapokaa na kutushambulia.”