Nehemiah 5:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilikunguta kibindo changu na kusema, “Kila mmoja asiyetimiza ahadi hii Mungu na amkungute, amtoe katika nyumba yake na katika kazi yake. Basi, akungutike na kubaki mikono mitupu.” Mkutano mzima ukaitikia, na kusema, “Amina” wakamsifu Mwenyezi-Mungu. Watu wakafanya kama walivyokuwa wameahidi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia nikakung’uta makunjo ya vazi langu na kusema, “Kila mtu ambaye hatatimiza ahadi hii, Mungu na amkung’ute hivi kutoka nyumba yake na katika mali yake. Basi mtu kama huyo akung’utiwe nje na aachwe bila kitu!” Waliposikia hili, mkutano wote ukasema, “Amen,” na wakamtukuza Mwenyezi Mungu. Nao watu wakafanya kama walivyokuwa wameahidi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena nikakung'uta nguo yangu, nikasema, Mungu na amkung'ute vivyo hivyo kila mtu nyumbani mwake, na kazini mwake, asiyeitimiza ahadi hiyo; naam, na akung'utwe vivyo hivyo, na kuwa hana kitu. Mkutano wote wakasema, Amina; wakamhimidi Bwana. Nao watu wakafanya kama ahadi hiyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilikung'uta kibindo changu na kusema, “Kila mmoja asiyetimiza ahadi hii Mungu na amkung'ute, amtoe katika nyumba yake na katika kazi yake. Basi, akung'utike na kubaki mikono mitupu.” Mkutano mzima ukaitikia, na kusema, “Amina;” wakamsifu Mwenyezi-Mungu. Watu wakafanya kama walivyokuwa wameahidi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia nikakung'uta makunjo ya vazi langu na kusema, “Kila mtu ambaye hatatimiza ahadi hii, Mungu na amkung'ute hivi kutoka katika nyumba yake na katika mali zake. Basi mtu wa jinsi hiyo na akung'utiwe nje na aachwe bila kitu!” Katika hili mkutano wote ukasema, “Amen” wakamtukuza BWANA. Nao watu wakafanya kama walivyokuwa wameahidi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia nikakung’uta makunjo ya vazi langu na kusema, “Kila mtu ambaye hatatimiza ahadi hii, Mungu na amkung’ute hivi kutoka nyumba yake na katika mali zake. Basi mtu wa namna hiyo akung’utiwe nje na aachwe bila kitu!” Waliposikia hili, mkutano wote ukasema, “Amen,” na wakamtukuza bwana. Nao watu wakafanya kama walivyokuwa wameahidi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena nikakung'uta nguo yangu, nikasema, Mungu na amkung'ute vivyo hivyo kila mtu nyumbani mwake, na kazini mwake, asiyeitimiza ahadi hiyo; naam, na akung'utwe vivyo hivyo, na kuwa hana kitu. Mkutano wote wakasema, Amina; wakamhimidi BWANA. Nao watu wakafanya kama walivyoahidi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilikunguta kibindo changu na kusema, “Kila mmoja asiyetimiza ahadi hii Mungu na amkungute, amtoe katika nyumba yake na katika kazi yake. Basi, akungutike na kubaki mikono mitupu.” Mkutano mzima ukaitikia, na kusema, “Amina” wakamsifu Mwenyezi-Mungu. Watu wakafanya kama walivyokuwa wameahidi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha nikaikung'uta mikunjo ya nguo zangu nikisema: Hivi ndivyo, Mungu atakavyomkung'uta kila mtu asiyelitimiza neno hili, atoke nyumbani mwake, nayo mapato yake yamtoke; kweli ndivyo, atakavyokung'utwa, awe pasipo kitu kabisa. Mkutano wote ukaitikia: Amin, kisha wakamsifu Bwana, watu wakafanya, kama walivyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena nikakung’uta nguo yangu, nikasema, Mungu na amkung’ute vivyo hivyo kila mtu nyumbani mwake, na kazini mwake, asiyeitimiza ahadi hiyo; naam, na akung’utwe vivyo hivyo, na kuwa hana kitu. Mkutano wote wakasema, Amina; wakamhimidi BWANA. Nao watu wakafanya kama ahadi hiyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nikakunguta upindo wa kanzu yangu na kusema: “Kila mumoja asiyetimiza ahadi hii Mungu amukungute, amutoe katika nyumba yake na katika kazi yake. Basi, akungutike na kubaki mikono mitupu.” Mukutano muzima wakaitikia, na kusema: “Amina”; wakamusifu Yawe. Watu wakafanya kama vile walivyokuwa wameahidi.