Nehemiah 5:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tangu wakati nilipoteuliwa kuwa mtawala wa nchi ya Yuda kwa miaka kumi na miwili yaani tangu mwaka wa ishirini mpaka mwaka wa thelathini na mbili wa kutawala kwa mfalme Artashasta, sikula chakula kinachostahili kuliwa na mtawala, wala ndugu zangu hawakufanya hivyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zaidi ya hayo, kutoka mwaka wa ishirini wa Mfalme Artashasta, wakati nilipoteuliwa kuwa mtawala wao katika nchi ya Yuda, hadi mwaka wake wa thelathini na mbili, yaani miaka kumi na mbili, mimi wala ndugu zangu hatukula chakula ambacho kwa kawaida hupewa watawala.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena tangu wakati huo nilipowekwa kuwa liwali wao katika nchi ya Yuda, tangu mwaka wa ishirini hata mwaka wa thelathini na mbili wa Artashasta mfalme, yaani, miaka kumi na miwili, mimi na ndugu zangu hatukula chakula cha liwali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tangu wakati nilipoteuliwa kuwa mtawala wa nchi ya Yuda kwa miaka kumi na miwili yaani tangu mwaka wa ishirini mpaka mwaka wa thelathini na mbili wa kutawala kwa mfalme Artashasta, sikula chakula kinachostahili kuliwa na mtawala, wala ndugu zangu hawakufanya hivyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zaidi ya hayo, kutoka mwaka wa ishirini wa Mfalme Artashasta, wakati nilipoteuliwa kuwa mtawala wao katika nchi ya Yuda, mpaka mwaka wake wa thelathini na mbili, yaani miaka kumi na miwili, mimi wala ndugu zangu hatukula chakula ambacho kwa kawaida hupewa watawala.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zaidi ya hayo, kutoka mwaka wa ishirini wa Mfalme Artashasta, wakati nilipoteuliwa kuwa mtawala wao katika nchi ya Yuda, mpaka mwaka wake wa thelathini na mbili, yaani miaka kumi na miwili, mimi wala ndugu zangu hatukula chakula ambacho kwa kawaida hupewa watawala.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena tangu wakati huo nilipowekwa kuwa mtawala wao katika nchi ya Yuda, tangu mwaka wa ishirini hadi mwaka wa thelathini na mbili wa Artashasta mfalme, yaani, miaka kumi na miwili, mimi na ndugu zangu hatukula chakula cha mtawala.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tangu wakati nilipoteuliwa kuwa mtawala wa nchi ya Yuda kwa miaka kumi na miwili yaani tangu mwaka wa ishirini mpaka mwaka wa thelathini na mbili wa kutawala kwa mfalme Artashasta, sikula chakula kinachostahili kuliwa na mtawala, wala ndugu zangu hawakufanya hivyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tangu siku ile, mfalme aliponiweka kuwa mtawala nchi kwao katika nchi ya Yuda, ni tangu mwaka wa ishirini hata mwaka wa thelathini na mbili wa mfalme Artasasta, hii miaka kumi na miwili, wala mimi wala ndugu zangu hatukula chakula cha mtawala nchi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena tangu wakati huo nilipowekwa kuwa liwali wao katika nchi ya Yuda, tangu mwaka wa ishirini hata mwaka wa thelathini na mbili wa Artashasta mfalme, yaani, miaka kumi na miwili, mimi na ndugu zangu hatukula chakula cha liwali.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tangu wakati nilipochaguliwa kuwa mutawala wa inchi ya Yuda kwa miaka kumi na miwili ni kusema tangu mwaka wa makumi mbili mpaka mwaka wa makumi tatu na mbili wa utawala kwa mufalme Artasasta, sikukula chakula kinachostahili kukuliwa na mutawala, wala wandugu zangu hawakufanya hivyo.