Nehemiah 5:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watawala walionitangulia walikuwa mzigo mzito kwa watu wakiwadai chakula na divai, mbali na kuwadai kuwalipa sarafu za uzito wa shekeli arubaini za fedha. Hata watumishi wao waliwadhulumu watu. Bali, mimi sikufanya hivyo, kwani nilimcha Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini watawala wa mwanzoni, wale walionitangulia, waliwalemea watu na kuchukua kutoka kwao shekeli arobaini za fedha, pamoja na chakula na mvinyo. Wasaidizi wao pia walijifanya wakuu juu ya watu. Lakini kwa kumheshimu Mungu sikufanya hivyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini maliwali wa kwanza walionitangulia, wakawalemea watu, wakawatwalia chakula na mvinyo, zaidi ya shekeli arobaini za fedha; tena watumwa wao nao wakatawala juu ya watu; lakini mimi sikufanya hivyo, kwa kuwa nalimcha Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watawala walionitangulia walikuwa mzigo mzito kwa watu wakiwadai chakula na divai, mbali na kuwadai kuwalipa sarafu za uzito wa shekeli arubaini za fedha. Hata watumishi wao waliwadhulumu watu. Bali, mimi sikufanya hivyo, kwani nilimcha Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini watawala wa mwanzoni, wale walionitangulia, waliwalemea watu na kuchukua kutoka kwao shekeli arobaini za fedha pamoja na chakula na mvinyo. Wasaidizi wao pia walipata nafasi ya kufaidi watu. Lakini kwa kumheshimu Mungu sikufanya hivyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini watawala wa mwanzoni, wale walionitangulia, waliwalemea watu na kuchukua kutoka kwao shekeli arobaini za fedha, pamoja na chakula na mvinyo. Wasaidizi wao pia walijifanya wakuu juu ya watu. Lakini kwa kumheshimu Mungu sikufanya hivyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini watawala wa kwanza walionitangulia, wakawalemea watu, wakawatwalia chakula na mvinyo, zaidi ya shekeli arobaini za fedha; tena hata watumishi wao nao wakawatawala watu; lakini mimi sikufanya hivyo, kwa kuwa nilimcha Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watawala walionitangulia walikuwa mzigo mzito kwa watu wakiwadai chakula na divai, mbali na kuwadai kuwalipa sarafu za uzito wa shekeli arubaini za fedha. Hata watumishi wao waliwadhulumu watu. Bali, mimi sikufanya hivyo, kwani nilimcha Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wenye amri walionitangulia waliwalemeza watu wakichukua kwao kila siku chakula na mvinyo za fedha arobaini na zaidi; vijana wao nao waliwakorofisha watu. Lakini mimi sikufanya kama hayo kwa kumwogopa Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini maliwali wa kwanza walionitangulia, wakawalemea watu, wakawatwalia chakula na mvinyo, zaidi ya shekeli arobaini za fedha; tena watumwa wao nao wakatawala juu ya watu; lakini mimi sikufanya hivyo, kwa kuwa nalimcha Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watawala walionitangulia walikuwa muzigo muzito kwa watu wakiwadai chakula na divai. Zaidi ya hiyo waliwalipisha vikoroti makumi ine vya feza. Hata watumishi wao waliwatesa watu. Lakini, mimi sikufanya hivyo, maana nilimwogopa Mungu.