Nehemiah 5:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila siku, ili kuwalisha watu hao, nilichinjiwa dume mmoja na kondoo safi sita na kuku. Kila baada ya siku kumi nilitoa kwa wingi viriba vya divai. Lakini licha ya haya yote, kwa kuwa watu walikuwa na mzigo mzito wa kubeba kila siku, sikutaka posho ya ziada.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila siku niliandaliwa maksai mmoja, kondoo sita wazuri, na kuku, na mvinyo wa kila aina kwa wingi kila baada ya siku kumi. Licha ya mambo haya yote, sikudai chakula kilichokuwa fungu la mtawala, kwa sababu madai yalikuwa mazito sana kwa watu hawa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, maandalio yaliyoandaliwa kwa siku moja yalikuwa ng'ombe mmoja, na kondoo wazuri sita; tena nikaandaliwa kuku, na mara moja katika siku kumi akiba ya mvinyo ya namna zote; wala kwa hayo yote sikukidai chakula cha liwali, kwa kuwa utumwa ulikuwa mzito juu ya watu hao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila siku, ili kuwalisha watu hao, nilichinjiwa dume mmoja na kondoo safi sita na kuku. Kila baada ya siku kumi nilitoa kwa wingi viriba vya divai. Lakini licha ya haya yote, kwa kuwa watu walikuwa na mzigo mzito wa kubeba kila siku, sikutaka posho ya ziada.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila siku niliandaliwa maksai mmoja, kondoo sita wazuri na kuku na mvinyo wa kila aina kwa wingi kila baada ya siku kumi. Licha ya mambo haya yote, sikudai chakula kilichokuwa fungu la mtawala, kwa sababu madai yalikuwa mazito sana kwa watu hawa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila siku niliandaliwa maksai mmoja, kondoo sita wazuri, na kuku, na mvinyo wa kila aina kwa wingi kila baada ya siku kumi. Licha ya mambo haya yote, sikudai chakula kilichokuwa fungu la mtawala, kwa sababu madai yalikuwa mazito sana kwa watu hawa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, maandalizi ya chakula yaliyoandaliwa kila siku yalikuwa ng'ombe mmoja na kondoo sita wazuri; tena nikaandaliwa kuku, na mara moja katika siku kumi akiba ya mvinyo ya namna zote; wala kwa hayo yote sikudai marupurupu ya chakula cha mtawala, kwa kuwa watu walikuwa wamebeba mzigo mzito.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila siku, ili kuwalisha watu hao, nilichinjiwa dume mmoja na kondoo safi sita na kuku. Kila baada ya siku kumi nilitoa kwa wingi viriba vya divai. Lakini licha ya haya yote, kwa kuwa watu walikuwa na mzigo mzito wa kubeba kila siku, sikutaka posho ya ziada.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Navyo vyakula vilivyoandaliwa vya kila siku moja, vilikuwa ng'ombe mmoja na kondoo sita waliochaguliwa vema na kuku pia, tena kila siku kumi mvinyo nyingi za kila namna. Kwa hayo yote sikutaka chakula cha mtawala nchi, kwani utumishi uliwalemea watu hawa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, maandalio yaliyoandaliwa kwa siku moja yalikuwa ng’ombe mmoja, na kondoo wazuri sita; tena nikaandaliwa kuku, na mara moja katika siku kumi akiba ya mvinyo ya namna zote; wala kwa hayo yote sikukidai chakula cha liwali, kwa kuwa utumwa ulikuwa mzito juu ya watu hao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila siku, kwa kuwalisha watu hao, nilichinjiwa ngombe dume mumoja na kondoo safi sita na kuku. Kila mara kisha siku kumi nilitoa divai kwa wingi. Lakini zaidi ya haya yote, kwa sababu watu walikuwa na muzigo muzito wa kubeba kila siku, sikutaka posho ya zaidi.