Nehemiah 5:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nikasema, “Kulingana na uwezo tulio nao, tumekuwa tukiwanunua tena ndugu zetu Wayahudi waliokuwa wameuzwa kwa watu wa mataifa mengine. Lakini sasa hata mnawauza ndugu zenu, nasi tunalazimika kuwanunua!” Basi walinyamaza kimya, bila kuwa na la kujibu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
nikasema: “Kulingana na uwezo wetu, tumewakomboa ndugu zetu Wayahudi waliokuwa wameuzwa kwa watu wasioamini. Sasa mnawauza ndugu zenu, ili wauzwe tena kwetu!” Wakanyamaza, kwa sababu hawakupata chochote cha kusema.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikawaambia, Sisi kwa kadiri ya uwezo wetu tumewakomboa ndugu zetu Wayahudi, waliouzwa kwa makafiri; na ninyi mnataka kuwauza ndugu zenu, tena kuwauza ili sisi tuwanunue? Wakanyamaza kimya, wasiweze kusema neno lo lote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nikasema, “Kulingana na uwezo tulio nao, tumekuwa tukiwanunua tena ndugu zetu Wayahudi waliokuwa wameuzwa kwa watu wa mataifa mengine. Lakini sasa hata mnawauza ndugu zenu, nasi tunalazimika kuwanunua!” Basi walinyamaza kimya, bila kuwa na la kujibu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
na kusema: “Kulingana na uwezo wetu, tumewakomboa ndugu zetu Wayahudi waliokuwa wameuzwa kwa Mataifa. Sasa mnawauza ndugu zenu, ili wauzwe tena kwetu!” Walinyamaza kimya, kwa sababu hawakupata cho chote cha kusema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
na kusema: “Kulingana na uwezo wetu, tumewakomboa ndugu zetu Wayahudi waliokuwa wameuzwa kwa watu wasioamini. Sasa mnawauza ndugu zenu, ili wauzwe tena kwetu!” Walinyamaza kimya, kwa sababu hawakupata chochote cha kusema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikawaambia, Sisi kwa kadiri ya uwezo wetu tumewakomboa ndugu zetu Wayahudi, waliouzwa kwa makafiri; na ninyi mnataka kuwauza ndugu zenu, tena kuwauza ili sisi tuwanunue? Wakanyamaza kimya, wasiweze kusema neno lolote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nikasema, “Kulingana na uwezo tulio nao, tumekuwa tukiwanunua tena ndugu zetu Wayahudi waliokuwa wameuzwa kwa watu wa mataifa mengine. Lakini sasa hata mnawauza ndugu zenu, nasi tunalazimika kuwanunua!” Basi walinyamaza kimya, bila kuwa na la kujibu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nikawaambia: Sisi tuliwakomboa ndugu zetu wa Kiyuda wlaiouzwa kwa wamizimu, kama tulivyoweza; nanyi mtawauza ndugu zenu, waje kujiuza kwetu sisi! Wakanyamaza kimya, hawakuona la kujibu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikawaambia, Sisi kwa kadiri ya uwezo wetu tumewakomboa ndugu zetu Wayahudi, waliouzwa kwa makafiri; na ninyi mnataka kuwauza ndugu zenu, tena kuwauza ili sisi tuwanunue? Wakanyamaza kimya, wasiweze kusema neno lo lote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nikasema: “Kulingana na uwezo tunaokuwa nao, tumekuwa tukiwanunua tena wandugu zetu Wayuda waliokuwa wameuzishwa kwa watu wa mataifa mengine. Lakini sasa hata munawauzisha wandugu zenu, nasi tunalazimika kuwanunua!” Basi wakanyamaza kimya, bila kuwa na la kujibu.