Nehemiah 6:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilipokwenda nyumbani kwa Shemaya, mwana wa Delaya mwana wa Mehetabeli, ambaye hakuruhusiwa kutoka nyumbani, aliniambia, “Twende tukutane katika nyumba ya Mungu na milango yake tuifunge kwa sababu leo usiku wanakuja kukuua.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku moja nilienda nyumbani mwa Shemaya mwana wa Delaya, mwana wa Mehetabeli, aliyekuwa amefungwa ndani ya nyumba yake. Akasema, “Tukutane katika nyumba ya Mungu, ndani ya Hekalu, na tufunge milango ya Hekalu, kwa sababu watu wanakuja kukuua. Naam, wanakuja usiku kukuua.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikaingia nyumbani kwa Shemaya, mwana wa Delaya, mwana wa Mehetabeli, aliyekuwa amefungwa; naye akasema, Tukutane nyumbani mwa Mungu, ndani ya hekalu, tukaifunge milango ya hekalu; kwa maana watakuja kukuua; naam, wakati wa usiku watakuja kukuua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilipokwenda nyumbani kwa Shemaya, mwana wa Delaya mwana wa Mehetabeli, ambaye hakuruhusiwa kutoka nyumbani, aliniambia, “Twende tukutane katika nyumba ya Mungu na milango yake tuifunge kwa sababu leo usiku wanakuja kukuua.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku moja nilikwenda nyumbani kwa Shemaya mwana wa Delaya, mwana wa Mehetabeli, ambaye alikuwa amefungwa ndani ya nyumba yake. Akasema, “Tukutane katika nyumba ya Mungu, ndani ya Hekalu na tufunge milango ya Hekalu, kwa sababu watu wanakuja kukuua. Naam, usiku wanakuja kukuua.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku moja nilikwenda nyumbani kwa Shemaya mwana wa Delaya, mwana wa Mehetabeli, ambaye alikuwa amefungwa ndani ya nyumba yake. Akasema, “Tukutane katika nyumba ya Mungu, ndani ya Hekalu, na tufunge milango ya Hekalu, kwa sababu watu wanakuja kukuua. Naam, wanakuja usiku kukuua.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikaingia nyumbani kwa Shemaya, mwana wa Delaya, mwana wa Mehetabeli, aliyekuwa amefungwa kifungo cha nyumbani; naye akasema, Tukutane nyumbani mwa Mungu, ndani ya hekalu, na tuifunge milango ya hekalu; kwa kuwa watakuja kukuua; naam, wakati wa usiku watakuja kukuua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilipokwenda nyumbani kwa Shemaya, mwana wa Delaya mwana wa Mehetabeli, ambaye hakuruhusiwa kutoka nyumbani, aliniambia, “Twende tukutane katika nyumba ya Mungu na milango yake tuifunge kwa sababu leo usiku wanakuja kukuua.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi nikaenda kuingia nyumbani mwa Semaya, mwana wa Delaya, mwana wa Mehetabeli, naye alikuwa amefungiwa; akaniambia: Na tukutane Nyumbani mwa Mungu, katikati ya Jumba hilo, tuifunge milango ya Jumba hilo, kwani wako wanaokuja kukuua, nao watakuja usiku huu, wakuue.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikaingia nyumbani kwa Shemaya, mwana wa Delaya, mwana wa Mehetabeli, aliyekuwa amefungwa; naye akasema, Tukutane nyumbani mwa Mungu, ndani ya hekalu, tukaifunge milango ya hekalu; kwa maana watakuja kukuua; naam, wakati wa usiku watakuja kukuua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilipokwenda kwa Semaya mwana wa Delaya mujukuu wa Mehetabeli, ambaye hakuruhusiwa kutoka kwake, akaniambia: “Twende tukutane katika nyumba ya Mungu na milango yake tuifunge kwa sababu leo usiku watakuja kukuua.”