Nehemiah 6:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa bahati nzuri, nilingamua kuwa alikuwa hajatumwa na Mungu, bali alikuwa amekodishwa na Tobia na Sanbalati atangaze mabaya dhidi yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nilitambua kwamba Mungu hakumtuma, bali alitabiri dhidi yangu kwa sababu Tobia na Sanbalati walikuwa wamemwajiri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikatambua, na tazama, siye Mungu aliyemtuma; lakini amefanya unabii huu kinyume changu; nao Tobia na Sanbalati ndio waliomwajiri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa bahati nzuri, niling'amua kuwa alikuwa hajatumwa na Mungu, bali alikuwa amekodishwa na Tobia na Sanbalati atangaze mabaya dhidi yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nilitambua kwamba Mungu hakumtuma, bali alitabiri dhidi yangu kwa sababu Tobia na Sanbalati walikuwa wamemwajiri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nilitambua kwamba Mungu hakumtuma, bali alitabiri dhidi yangu kwa sababu Tobia na Sanbalati walikuwa wamemwajiri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikatambua, na tazama, si Mungu aliyemtuma; lakini amefanya unabii huu kinyume changu; kwa kuwa Tobia na Sanbalati ndio waliomwajiri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa bahati nzuri, nilingamua kuwa alikuwa hajatumwa na Mungu, bali alikuwa amekodishwa na Tobia na Sanbalati atangaze mabaya dhidi yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nalikuwa nimetambua, nikaona, ya kuwa siye Mungu aliyemtuma, aniambie huo ufumbuaji, ila Tobia na Sanibalati walikuwa wamempenyezea mali.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikatambua, na tazama, siye Mungu aliyemtuma; lakini amefanya unabii huu kinyume changu; nao Tobia na Sanbalati ndio waliomwajiri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nikatambua kwamba hakutumwa na Mungu, lakini alikuwa amelipwa na Tobia na Sanibalati atangaze mabaya juu yangu.