Nehemiah 6:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nikamwomba Mungu nikisema, “Ee Mungu, kumbuka yote waliyotenda Tobia na Sanbalati, hata yule Noadia, nabii mwanamke, na manabii wengine waliotaka kunifanya niogope.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ee Mungu wangu, wakumbuke Tobia na Sanbalati kwa sababu ya yale waliyotenda. Pia kumbuka nabii mke Noadia na manabii wengine ambao wamekuwa wakijaribu kunitisha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Uwakumbuke, Ee Mungu wangu, Tobia na Sanbalati sawasawa na hayo matendo yao, na yule nabii mke Noadia, na hao manabii waliosalia, waliotaka kuniogofya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nikamwomba Mungu nikisema, “Ee Mungu, kumbuka yote waliyotenda Tobia na Sanbalati, hata yule Noadia, nabii mwanamke, na manabii wengine waliotaka kunifanya niogope.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ee Mungu wangu, wakumbuke Tobia na Sanbalati kwa sababu ya yale waliyotenda, pia kumbuka nabii mke Noadia na manabii wengine ambao wamekuwa wakijaribu kunitisha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ee Mungu wangu, wakumbuke Tobia na Sanbalati kwa sababu ya yale waliyotenda. Pia kumbuka nabii mke Noadia na manabii wengine ambao wamekuwa wakijaribu kunitisha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Uwakumbuke, Ee Mungu wangu, Tobia na Sanbalati kulingana na hayo matendo yao, na yule nabii mwanamke Noadia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nikamwomba Mungu nikisema, “Ee Mungu, kumbuka yote waliyotenda Tobia na Sanbalati, hata yule Noadia, nabii mwanamke, na manabii wengine waliotaka kunifanya niogope.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mungu wangu, yakumbuke hayo matendo ya Tobia na ya Sanibalati! Mkumbuke naye mfumbuaji mke Noadia na wale wafumbuaji wengine waliotaka kuniogopesha!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Uwakumbuke, Ee Mungu wangu, Tobia na Sanbalati sawasawa na hayo matendo yao, na yule nabii mke Noadia, na hao manabii waliosalia, waliotaka kuniogofya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nikamwomba Mungu nikisema: “Ee Mungu, kumbuka mambo yote Tobia na Sanibalati waliyotenda, hata yule Noadia, nabii mwanamuke, na manabii wengine waliotaka kuniogopesha.”