Nehemiah 6:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na barua yenyewe iliandikwa ifuatavyo: “Kuna habari zilizoenezwa miongoni mwa mataifa jirani, na Geshemu anathibitisha habari hizi, kuwa wewe pamoja na Wayahudi wenzako mnakusudia kuasi. Hii ndiyo sababu mnaujenga upya ukuta. Kulingana na habari hizo, wewe unakusudia kuwa mfalme wao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
iliyokuwa imeandikwa: “Habari imeenezwa miongoni mwa mataifa, naye Geshemu anasema kwamba ni kweli, kuwa wewe na Wayahudi mnapanga njama ya kuasi, ndiyo sababu mnajenga ukuta. Zaidi ya hayo, kufuatana na taarifa hizi, karibuni utakuwa mfalme wao,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nayo yakaandikwa humo, Habari imeenea katika mataifa, naye Geshemu asema neno lilo hilo, ya kwamba wewe na Wayahudi mwakusudi kuasi; ndiyo sababu waujenga huo ukuta; nawe wataka kuwamiliki, ndivyo wasemavyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na barua yenyewe iliandikwa ifuatavyo: “Kuna habari zilizoenezwa miongoni mwa mataifa jirani, na Geshemu anathibitisha habari hizi, kuwa wewe pamoja na Wayahudi wenzako mnakusudia kuasi. Hii ndiyo sababu mnaujenga upya ukuta. Kulingana na habari hizo, wewe unakusudia kuwa mfalme wao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
iliyokuwa imeandikwa: “Habari imeenezwa miongoni mwa mataifa naye Geshemu anasema kwamba ni kweli, kuwa wewe na Wayahudi mnafanya hila ya kuasi, ndiyo sababu mnajenga ukuta. Zaidi ya hayo, kwa kufuatana na taarifa hizi karibu utakuwa mfalme wao
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
iliyokuwa imeandikwa: “Habari imeenezwa miongoni mwa mataifa, naye Geshemu anasema kwamba ni kweli, kuwa wewe na Wayahudi mnafanya hila ya kuasi, ndiyo sababu mnajenga ukuta. Zaidi ya hayo, kufuatana na taarifa hizi, karibuni utakuwa mfalme wao,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nayo yakaandikwa humo, Habari imeenea katika mataifa, naye Geshemu asema neno lilo hilo, ya kwamba wewe na Wayahudi mnakusudia kuasi; ndiyo sababu unaujenga huo ukuta; nawe unataka kuwamiliki, ndivyo wasemavyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na barua yenyewe iliandikwa ifuatavyo: “Kuna habari zilizoenezwa miongoni mwa mataifa jirani, na Geshemu anathibitisha habari hizi, kuwa wewe pamoja na Wayahudi wenzako mnakusudia kuasi. Hii ndiyo sababu mnaujenga upya ukuta. Kulingana na habari hizo, wewe unakusudia kuwa mfalme wao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Humo yalikuwa yameandikwa haya: Katika wamizimu yanasimuliwa, naye Gasemu anayasema, ya kuwa wewe na wayuda mnawaza kumwinukia mfalme, kwa sababu hii unalijenga boma, wewe upate kuwa mfalme wao, na mengine kama hayo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nayo yakaandikwa humo, Habari imeenea katika mataifa, naye Geshemu asema neno lilo hilo, ya kwamba wewe na Wayahudi mwakusudi kuasi; ndiyo sababu waujenga huo ukuta; nawe wataka kuwamiliki, ndivyo wasemavyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na barua yenyewe iliandikwa hivi: Kuna habari zilizoenezwa kati ya mataifa jirani, na Gesemi anahakikisha habari hizi, kwamba wewe pamoja na Wayuda wenzako munakusudia kuasi. Hii ndiyo sababu munaujenga upya ukuta. Kulingana na habari hizo, wewe unakusudia kuwa mufalme wao.