Nehemiah 7:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
nikawaagiza, “Malango yasifunguliwe usiku kucha hadi jua linapokuwa limepanda. Kabla hawajaondoka walinzi ni lazima kufunga milango yote kwa makomeo yake. Teueni walinzi miongoni mwa wakazi wa mji wa Yerusalemu, kila mmoja awe mahali pake kukabiliana na nyumba yake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nikawaambia, “Malango ya Yerusalemu yasifunguliwe hadi jua litakapokuwa limepanda. Walinzi wa malango wakiwa bado kwenye zamu, waamuru wafunge milango na waweke makomeo. Pia wateueni wenyeji wa Yerusalemu wawe walinzi, kila mmoja kwenye lindo lake, na wengine karibu na nyumba zao wenyewe.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikawaambia, Yasifunguliwe malango ya Yerusalemu kabla halijachomoza jua; nao walinzi wangali wakisimama bado, waifunge milango, mkaikaze; kisha wekeni walinzi wa zamu wa hao wakaao Yerusalemu, kila mtu na zamu yake, na kila mtu kuielekea nyumba yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
nikawaagiza, “Malango yasifunguliwe usiku kucha hadi jua linapokuwa limepanda. Kabla hawajaondoka walinzi ni lazima kufunga milango yote kwa makomeo yake. Teueni walinzi miongoni mwa wakazi wa mji wa Yerusalemu, kila mmoja awe mahali pake kukabiliana na nyumba yake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nikawaambia, “Malango ya Yerusalemu yasifunguliwe mpaka jua litakapokuwa limepanda. Wakati walinzi wa malango wakiwa kwenye zamu, wafunge milango na waweke makomeo. Pia wateueni wenyeji wa Yerusalemu wawe walinzi, kila mmoja kwenye lindo lake na wengine karibu na nyumba zao wenyewe.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nikawaambia, “Malango ya Yerusalemu yasifunguliwe mpaka jua litakapokuwa limepanda. Walinzi wa malango wakiwa bado kwenye zamu, waamuru wafunge milango na waweke makomeo. Pia wateueni wenyeji wa Yerusalemu wawe walinzi, kila mmoja kwenye lindo lake, na wengine karibu na nyumba zao wenyewe.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikawaambia, Yasifunguliwe malango ya Yerusalemu kabla jua halijachomoza; na kabla walinzi hawajaondoka waifunge milango, mkaikaze; kisha wekeni walinzi wa zamu wa hao wakaao Yerusalemu, kila mtu na zamu yake, na kila mtu kuielekea nyumba yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
nikawaagiza, “Malango yasifunguliwe usiku kucha hadi jua linapokuwa limepanda. Kabla hawajaondoka walinzi ni lazima kufunga milango yote kwa makomeo yake. Teueni walinzi miongoni mwa wakazi wa mji wa Yerusalemu, kila mmoja awe mahali pake kukabiliana na nyumba yake.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikawaambia: Malango ya Yerusalemu yasifunguliwe, mpaka jua liwake na nguvu; tena walinzi wakingali wanasimama, malango yafungwe na kutiwa makomeo. Tena mweke wenyeji wa Yerusalemu kuwa walinzi kila mtu na zamu yake ya kulinda hapo panapoielekea nyumba yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikawaambia, Yasifunguliwe malango ya Yerusalemu kabla halijachomoza jua; nao walinzi wangali wakisimama bado, waifunge milango, mkaikaze; kisha wekeni walinzi wa zamu wa hao wakaao Yerusalemu, kila mtu na zamu yake, na kila mtu kuielekea nyumba yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
nikawaagiza: “Milango isifunguliwe usiku kucha mpaka jua linapokuwa limepanda. Mbele ya kuondoka kwa walinzi ni lazima kufunga milango yote kwa vifungio vyake. Muchague walinzi kati ya wakaaji wa muji wa Yerusalema, kila mumoja akuwe kwa nafasi yake kuelekeana na nyumba yake.”