Nehemiah 7:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu akanipa moyo kuwakusanya viongozi na watu ili kujua koo zao. Nikapata kitabu cha koo za watu waliorudi toka uhamishoni mara ya kwanza, na hawa wafuatao ndio waliokuwa wameorodheshwa ndani yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Mungu wangu akaweka moyoni mwangu kuwakusanya wakuu, maafisa na watu kwa ajili ya kuorodheshwa kulingana na jamaa zao. Nilikuta orodha ya vizazi ya wale waliokuwa wa kwanza kurudi toka utumwani. Haya ndio niliyokuta yameandikwa humo:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mungu wangu akanitia moyoni mwangu, kwamba niwakusanye wakuu na mashehe, na watu, ili wahesabiwe kwa nasaba. Nikakiona kitabu cha vizazi vya hao waliokwea hapo kwanza, nikaona ya kwamba imeandikwa humo;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu akanipa moyo kuwakusanya viongozi na watu ili kujua koo zao. Nikapata kitabu cha koo za watu waliorudi toka uhamishoni mara ya kwanza, na hawa wafuatao ndio waliokuwa wameorodheshwa ndani yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo Mungu wangu akaweka moyoni mwangu kuwakusanya wakuu, maafisa na watu wa kawaida kwa ajili ya kuorodheshwa kulingana na jamaa zao. Nilikuta orodha ya vizazi iliyoandikwa ya wale waliokuwa wa kwanza kurudi toka utumwani. Haya ndiyo niliyokuta yameandikwa humo:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo Mungu wangu akaweka moyoni mwangu kuwakusanya wakuu, maafisa na watu wa kawaida kwa ajili ya kuorodheshwa kulingana na jamaa zao. Nilikuta orodha ya vizazi ya wale waliokuwa wa kwanza kurudi toka utumwani. Haya ndiyo niliyokuta yameandikwa humo:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mungu wangu akatia wazo moyoni mwangu, kwamba niwakusanye wakuu na maofisa, na watu, ili wahesabiwe kwa nasaba. Nikakiona kitabu cha vizazi vya hao waliokwea hapo kwanza, nikaona ya kwamba imeandikwa humo;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu akanipa moyo kuwakusanya viongozi na watu ili kujua koo zao. Nikapata kitabu cha koo za watu waliorudi toka uhamishoni mara ya kwanza, na hawa wafuatao ndio waliokuwa wameorodheshwa ndani yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mungu akanitia moyoni, niwakusanye wakuu wa miji na watawalaji nao watu, waandikwe milango yao. Nikaona chuo kilichoandikwa udugu wao walionza kurudi na kupanda huku, nikaona yameandikwa haya:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mungu wangu akanitia moyoni mwangu, kwamba niwakusanye wakuu na mashehe, na watu, ili wahesabiwe kwa nasaba. Nikakiona kitabu cha vizazi vya hao waliokwea hapo kwanza, nikaona ya kwamba imeandikwa humo;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu akanipa moyo kuwakusanya viongozi na watu kwa kujua ukoo zao. Nikapata kitabu cha ukoo za watu waliorudi toka katika uhamisho mara ya kwanza, na hawa ndio waliokuwa wameandikwa ndani yake.