Nehemiah 7:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale waliokuwa uhamishoni kule Babuloni, walirudi mjini Yerusalemu na nchini Yuda, kila mmoja akarudi mjini kwake. Jamaa zao walikuwa wamekaa Babuloni tangu mfalme Nebukadneza alipowahamishia huko wakiwa mateka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hawa ndio wana wa wilaya, waliokwea kutoka katika ule uhamisho wa hao waliokuwa wamechukuliwa, ambao Nebukadreza,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale waliokuwa uhamishoni kule Babuloni, walirudi mjini Yerusalemu na nchini Yuda, kila mmoja akarudi mjini kwake. Jamaa zao walikuwa wamekaa Babuloni tangu mfalme Nebukadneza alipowahamishia huko wakiwa mateka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hawa ndio watu wa jimbo waliorudi kutoka utumwani uhamishoni walikokuwa wamepelekwa na Mfalme Nebukadneza wa Babeli (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hawa ndio wana wa wilaya, waliokwea kutoka katika ule uhamisho wa hao waliokuwa wamechukuliwa, ambao Nebukadneza, mfalme wa Babeli, aliwachukua mateka, nao wakarudi Yerusalemu na Yuda, kila mtu mjini kwake;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale waliokuwa uhamishoni kule Babuloni, walirudi mjini Yerusalemu na nchini Yuda, kila mmoja akarudi mjini kwake. Jamaa zao walikuwa wamekaa Babuloni tangu mfalme Nebukadneza alipowahamishia huko wakiwa mateka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hawa ndio watu waliokaa majimboni waliporudi kutoka mafungoni kwenye kutekwa; ndio wao, Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, aliowateka na kuwahamisha, nao wakapata kurudi Yerusalemu na Yuda, kila mtu mjini kwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hawa ndio wana wa wilaya, waliokwea kutoka katika ule uhamisho wa hao waliokuwa wamechukuliwa, ambao Nebukadreza, mfalme wa Babeli, aliwachukua mateka, nao wakarudi Yerusalemu na Yuda, kila mtu mjini kwake;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale waliokuwa katika uhamisho kule Babeli, walirudi Yerusalema na katika inchi ya Yuda, kila mumoja akarudi katika muji wake. Jamaa zao walikuwa wamekaa Babeli tangu mufalme Nebukadneza alipowahamishia kule wakiwa watumwa.