Nehemiah 7:64 — Compare Translations

10 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hao walitafuta orodha yao kati ya wengine walioorodheshwa katika kumbukumbu za koo, lakini ukoo wao haukuwemo. Kwa hiyo hawakuruhusiwa kutiwa katika huduma ya ukuhani kwani walihesabiwa kuwa najisi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa ukuhani, kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hao waliitafuta orodha yao miongoni mwa wale waliohesabiwa kwa nasaba, wasionekane; kwa hiyo walihesabiwa kuwa na unajisi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hao walitafuta orodha yao kati ya wengine walioorodheshwa katika kumbukumbu za koo, lakini ukoo wao haukuwemo. Kwa hiyo hawakuruhusiwa kutiwa katika huduma ya ukuhani kwani walihesabiwa kuwa najisi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hawa walitafuta katika orodha ya jamii zao, lakini hawakuonekana kwa hiyo waliondolewa katika ukuhani kama watu najisi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani, kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hao waliitafuta orodha yao miongoni mwa wale waliohesabiwa kwa nasaba, wasionekane; kwa hiyo walihesabiwa kuwa na unajisi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hao walitafuta orodha yao kati ya wengine walioorodheshwa katika kumbukumbu za koo, lakini ukoo wao haukuwemo. Kwa hiyo hawakuruhusiwa kutiwa katika huduma ya ukuhani kwani walihesabiwa kuwa najisi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hawa walikitafuta kitabu chao cha udugu wao, lakini hawakukiona, kwa hiyo wakakatazwa utambikaji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)