Nehemiah 7:70 — Compare Translations

10 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadhi ya wakuu wa koo walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala wa mkoa alitoa kilo 8 za dhahabu, mabirika 50, mavazi 530.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baadhi ya viongozi wa jamaa walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala alikabidhi kwenye hazina darkoni elfu moja za dhahabu, mabakuli hamsini, na mavazi mia tano na thelathini ya makuhani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na baadhi ya wakuu wa mbari za mababa walitoa mali kwa ajili ya kazi hii. Yule Tirshatha akatoa kwa ajili ya hazina darkoni
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadhi ya wakuu wa koo walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala wa mkoa alitoa kilo 8 za dhahabu, mabirika 50, mavazi 530.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baadhi ya wakuu wa mbari walichangia kazi ya ujenzi. Tirshatha alikabidhi kwenye hazina darkoni 1,000 za dhahabu, mabakuli 50 na mavazi 530 kwa ajili ya makuhani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baadhi ya viongozi wa jamaa walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala alikabidhi kwenye hazina darkoni 1,000 za dhahabu, mabakuli 50, na mavazi 530 kwa ajili ya makuhani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na baadhi ya wakuu wa mbari za mababa walitoa mali kwa ajili ya kazi hii. Yule Tirshatha akatoa kwa ajili ya hazina darkoni, za dhahabu elfu moja, na mabeseni hamsini, na mavazi ya makuhani mia tano na thelathini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadhi ya wakuu wa koo walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala wa mkoa alitoa kilo 8 za dhahabu, mabirika 50, mavazi 530.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakuu wengine wa milango wakatoa vipaji vya kufanyia hizo kazi za jengo: mtawala nchi alitoa na kutia katika kilimbiko: vipande vya dhahabu vilivyoitwa Dariko 1000, ndio shilingi kama 40000, na vyano 50 na mavazi ya watambikaji 530.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na baadhi ya wakuu wa mbari za mababa walitoa mali kwa ajili ya kazi hii. Yule Tirshatha akatoa kwa ajili ya hazina darkoni za dhahabu elfu moja, na mabakuli hamsini, na mavazi ya makuhani mia tano na thelathini.