Nehemiah 8:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa rudini nyumbani mkafanye sherehe, mle vinono na kunywa divai nzuri, lakini kumbukeni kuwapelekea wale ambao hawana cha kutosha; kwani leo ni siku takatifu kwa Bwana wetu. Msihuzunike kwa sababu furaha anayowajalia Mwenyezi-Mungu itawapeni nguvu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nehemia akasema, “Nendeni mkafurahie chakula kizuri na vinywaji vitamu, na mpeleke sehemu kwa wale ambao hawana chochote cha kula. Siku hii ni takatifu kwa Mwenyezi Mungu. Msihuzunike, kwa kuwa furaha ya Mwenyezi Mungu ni nguvu zenu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha akawaambia, Enendeni zenu, mle kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye asiyewekewa kitu; maana siku hii ni takatifu kwa Bwana wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu zenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa rudini nyumbani mkafanye sherehe, mle vinono na kunywa divai nzuri, lakini kumbukeni kuwapelekea wale ambao hawana cha kutosha; kwani leo ni siku takatifu kwa Bwana wetu. Msihuzunike kwa sababu furaha anayowajalia Mwenyezi-Mungu itawapeni nguvu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nehemia akasema, “Nendeni mkafurahie chakula kizuri na vinywaji vitamu, na mpeleke sehemu kwa wale ambao hawana cho chote cha kula. Siku hii ni takatifu kwa BWANA. Msihuzunike, kwa kuwa furaha ya BWANA ni nguvu zenu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nehemia akasema, “Nendeni mkafurahie chakula kizuri na vinywaji vitamu, na mpeleke sehemu kwa wale ambao hawana chochote cha kula. Siku hii ni takatifu kwa bwana. Msihuzunike, kwa kuwa furaha ya bwana ni nguvu zenu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha akawaambia, Nendeni zenu, mle kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye asiyekuwa na kitu; maana siku hii ni takatifu kwa BWANA wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya BWANA ni nguvu zenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa rudini nyumbani mkafanye sherehe, mle vinono na kunywa divai nzuri, lakini kumbukeni kuwapelekea wale ambao hawana cha kutosha; kwani leo ni siku takatifu kwa Bwana wetu. Msihuzunike kwa sababu furaha anayowajalia Mwenyezi-Mungu itawapeni nguvu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaendelea akiwaambia: Haya! Nendeni, mle vinono pamoja na kunywa vinywaji vitamu! Nao wakosao vya kujiandalia wapelekeeni magawio! Kwani siku ya leo ni siku takatifu ya Mungu wetu. Kwa hiyo msisikitike! Kwani kumfurahia Bwana ndiko kunakowapa nguvu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha akawaambia, Enendeni zenu, mle kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye asiyewekewa kitu; maana siku hii ni takatifu kwa BWANA wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya BWANA ni nguvu zenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa murudi kwa nyumba mufanye sherehe, mukule vyakula na kunywa divai nzuri, lakini mukumbuke kuwapelekea wale ambao hawana kitu cha kutosha; maana leo ni siku takatifu kwa Bwana wetu. Musihuzunike kwa sababu furaha Yawe anayowajalia itawapa nguvu.”