Nehemiah 8:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wote wakarudi nyumbani kwao kula na kunywa; wakifurahi na kuwagawia wengine chakula kwa kuwa waliyaelewa yote waliyotangaziwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha watu wote wakaondoka kwenda kula na kunywa, na kupeana sehemu ya chakula, na wakaadhimisha kwa furaha kubwa, kwa sababu sasa walifahamu maneno yale waliyokuwa wameelezwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na watu wote wakaenda zao kula na kunywa, na kuwapelekea watu sehemu, na kufanya furaha nyingi, kwa sababu walikuwa wameyafahamu maneno yale waliyohubiriwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wote wakarudi nyumbani kwao kula na kunywa; wakifurahi na kuwagawia wengine chakula kwa kuwa waliyaelewa yote waliyotangaziwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha watu wote wakaondoka kwenda kula na kunywa na kuwapelekea watu sehemu ya chakula na wakaadhimisha kwa furaha kubwa, kwa sababu sasa wamefahamu maneno yale waliyokuwa wameelezwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha watu wote wakaondoka kwenda kula na kunywa, na kupeana sehemu ya chakula, na wakaadhimisha kwa furaha kubwa, kwa sababu sasa walifahamu maneno yale waliyokuwa wameelezwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na watu wote wakaenda zao kula na kunywa, na kuwapelekea watu sehemu, na kufanya furaha nyingi, kwa sababu walikuwa wameyafahamu maneno yale waliyohubiriwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wote wakarudi nyumbani kwao kula na kunywa; wakifurahi na kuwagawia wengine chakula kwa kuwa waliyaelewa yote waliyotangaziwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, watu wote walipokwenda, wale, wanywe, wapeleke magawio, wafanye sikukuu yenye furaha kubwa, kwa kuwa waliyatambua hayo maneno, waliyojulishwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na watu wote wakaenda zao kula na kunywa, na kuwapelekea watu sehemu, na kufanya furaha nyingi, kwa sababu walikuwa wameyafahamu maneno yale waliyohubiriwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wote wakarudi kwao kwa kula na kunywa, wakifurahi na kuwagawanyia wengine chakula kwa sababu walielewa yote waliyotangaziwa.