Nehemiah 8:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kesho yake, wakuu wa koo pamoja na makuhani na Walawi wakakusanyika kwa Ezra mwandishi, ili kujifunza sheria.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika siku ya pili ya mwezi, wakuu wa jamaa zote, pamoja na makuhani na Walawi, walikusanyika wakimzunguka Ezra mwandishi ili wapate kusikiliza kwa makini maneno ya Torati.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata siku ya pili wakuu wa mbari za mababa za watu wote, na makuhani, na Walawi, wakamkusanyikia Ezra, mwandishi, ili wapate kuyasikiliza maneno ya torati.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kesho yake, wakuu wa koo pamoja na makuhani na Walawi wakakusanyika kwa Ezra mwandishi, ili kujifunza sheria.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika siku ya pili ya mwezi, wakuu wa mbari zote, pamoja na makuhani na Walawi, walikusanyika wakimzunguka Ezra mwandishi wapate kusikiliza kwa makini maneno ya Sheria.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika siku ya pili ya mwezi, wakuu wa mbari zote, pamoja na makuhani na Walawi, walikusanyika wakimzunguka Ezra mwandishi ili wapate kusikiliza kwa makini maneno ya Torati.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata siku ya pili wakuu wa mbari za mababu za watu wote, na makuhani, na Walawi, wakamkusanyikia Ezra, mwandishi, ili wapate kujifunza maneno ya torati.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kesho yake, wakuu wa koo pamoja na makuhani na Walawi wakakusanyika kwa Ezra mwandishi, ili kujifunza sheria.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ya pili wakuu wa milango ya watu wote na watambikaji na Walawi wakakusanyika kwa mwandishi Ezera, wajifundishe vema maneno ya Maonyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata siku ya pili wakuu wa mbari za mababa za watu wote, na makuhani, na Walawi, wakamkusanyikia Ezra, mwandishi, ili wapate kuyasikiliza maneno ya torati.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kesho yake, wakubwa wa ukoo pamoja na makuhani na Walawi wakakusanyika kwa Ezra mwandishi, kwa kujifunza Sheria.