Nehemiah 8:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, watu wakaenda kuleta matawi, wakajijengea vibanda kila mtu kwenye dari na kwenye baraza ya nyumba yake, kwenye baraza za nyumba ya Mungu, kwenye uwanja wa Lango la Maji na uwanja wa Lango la Efraimu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi watu wakaenda na kuleta matawi, nao wakajijengea vibanda juu ya paa za nyumba zao, katika nyua zao, katika nyua za nyumba ya Mungu, na katika uwanja karibu na Lango la Maji, na uwanja wa Lango la Efraimu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi watu wote wakatoka, wakayaleta, wakajifanyizia vibanda, kila mtu juu ya dari ya nyumba yake, na katika nyua zao, na katika nyua za nyumba ya Mungu, na katika uwanja wa lango la maji, na katika uwanja wa lango la Efraimu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, watu wakaenda kuleta matawi, wakajijengea vibanda kila mtu kwenye dari na kwenye baraza ya nyumba yake, kwenye baraza za nyumba ya Mungu, kwenye uwanja wa Lango la Maji na uwanja wa Lango la Efraimu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi watu wakaenda na kuleta matawi nao wakajijengea vibanda juu ya paa za nyumba zao, katika nyua zao, katika nyua za nyumba ya Mungu na katika uwanja karibu na Lango la Maji na uwanja wa Lango la Efraimu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi watu wakaenda na kuleta matawi, nao wakajijengea vibanda juu ya paa za nyumba zao, katika nyua zao, katika nyua za nyumba ya Mungu, na katika uwanja karibu na Lango la Maji na uwanja wa Lango la Efraimu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi watu wote wakatoka, wakayaleta, wakajitengenezea vibanda, kila mtu juu ya dari la nyumba yake, na katika nyua zao, na katika nyua za nyumba ya Mungu, na katika uwanja wa lango la maji, na katika uwanja wa lango la Efraimu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, watu wakaenda kuleta matawi, wakajijengea vibanda kila mtu kwenye dari na kwenye baraza ya nyumba yake, kwenye baraza za nyumba ya Mungu, kwenye uwanja wa Lango la Maji na uwanja wa Lango la Efraimu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, watu walipotoka, wakaleta matawi, wakajijengea vibanda kila mtu juu darini kwake napo penye nyua zao napo penye ua wa Nyumba ya Mungu napo penye uwanja ulioko kwenye lango la Maji napo penye uwanja ulioko kwenye lango la Efuraimu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi watu wote wakatoka, wakayaleta, wakajifanyizia vibanda, kila mtu juu ya dari ya nyumba yake, na katika nyua zao, na katika nyua za nyumba ya Mungu, na katika uwanja wa lango la maji, na katika uwanja wa lango la Efraimu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, watu wakaenda kuleta matawi, wakajenga vibanda kila mutu kwenye dari na kwenye baraza ya nyumba yake, kwenye baraza za nyumba ya Mungu, kwenye uwanja wa kiwanja cha Mulango wa Maji na kiwanja cha Mulango wa Efuraimu.