Nehemiah 8:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wote waliorudi kutoka uhamishoni wakatengeneza vibanda wakaishi humo. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza watu kuishi katika vibanda tangu wakati Yeshua, mwana wa Nuni alipokuwa akiishi. Watu walifurahi sana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jamii yote ya watu waliorudi kutoka utumwani wakajenga vibanda na kuishi ndani yake. Tangu wakati wa Yoshua mwana wa Nuni hadi siku ile, Waisraeli hawakuwahi kuiadhimisha namna hii. Furaha yao ilikuwa kubwa sana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mkutano wote wa watu, waliorudi kutoka nchi ya uhamisho wao, wakafanyiza vibanda, wakakaa katika vibanda hivyo; maana tokea siku za Yoshua, mwana wa Nuni, hata siku ile, wana wa Israeli hawakufanya hivyo. Pakawa na furaha kubwa sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wote waliorudi kutoka uhamishoni wakatengeneza vibanda wakaishi humo. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza watu kuishi katika vibanda tangu wakati Yeshua, mwana wa Nuni alipokuwa akiishi. Watu walifurahi sana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Jamii yote ya watu waliorudi kutoka utumwani wakajenga vibanda na kuishi ndani yake. Tangu wakati wa Yoshua mwana wa Nuni mpaka siku ile, Waisraeli hawakuwahi kuiadhimisha namna hii kama hivi. Furaha yao ilikuwa kubwa sana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jamii yote ya watu waliorudi kutoka utumwani wakajenga vibanda na kuishi ndani yake. Tangu wakati wa Yoshua mwana wa Nuni mpaka siku ile, Waisraeli hawakuwahi kuiadhimisha namna hii. Furaha yao ilikuwa kubwa sana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mkutano wote wa watu, waliorudi kutoka nchi ya uhamisho wao, wakatengeneza vibanda, wakakaa katika vibanda hivyo; maana tangu siku za Yoshua, mwana wa Nuni, hadi siku ile, wana wa Israeli hawakufanya hivyo. Pakawa na furaha kubwa sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wote waliorudi kutoka uhamishoni wakatengeneza vibanda wakaishi humo. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza watu kuishi katika vibanda tangu wakati Yeshua, mwana wa Nuni alipokuwa akiishi. Watu walifurahi sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo mkutano wao wote waliorudi mafungoni kwenye kutekwa wakajijengea vibanda, wakakaa vibandani; kwani tangu siku za Yosua, mwana wa Nuni, mpaka siku hiyo wana wa Isiraeli hawakufanya hivyo, ikawa furaha kubwa sana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mkutano wote wa watu, waliorudi kutoka nchi ya uhamisho wao, wakafanyiza vibanda, wakakaa katika vibanda hivyo; maana tokea siku za Yoshua, mwana wa Nuni, hata siku ile, wana wa Israeli hawakufanya hivyo. Pakawa na furaha kubwa sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wote waliorudi kutoka katika uhamisho wakatengeneza vibanda wakaishi ndani yake. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza watu kuishi katika vibanda tangu wakati Yesua mwana wa Nuni alipokuwa akiishi. Watu wakafurahi sana.