Nehemiah 8:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ezra, ambaye alikuwa kuhani, akaenda na kukileta kitabu cha sheria ya Mose mbele ya mkutano mzima, wanaume kwa wanawake na yeyote aliyeweza kuielewa hiyo sheria aliposikia. Siku hiyo ilikuwa ni siku ya kwanza ya mwezi wa saba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba, kuhani Ezra akaleta Torati mbele ya kusanyiko, ambamo walikuwamo wanaume, wanawake na watu wote walioweza kufahamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Ezra, kuhani, akaileta torati mbele ya kusanyiko, la wanaume na wanawake, na wote walioweza kusikia na kufahamu, siku ya kwanza na mwezi wa saba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ezra, ambaye alikuwa kuhani, akaenda na kukileta kitabu cha sheria ya Mose mbele ya mkutano mzima, wanaume kwa wanawake na yeyote aliyeweza kuielewa hiyo sheria aliposikia. Siku hiyo ilikuwa ni siku ya kwanza ya mwezi wa saba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba kuhani Ezra akaleta Sheria mbele ya kusanyiko, ambamo walikuwemo wanaume, wanawake na watu wote walioweza kufahamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba, kuhani Ezra akaleta Torati mbele ya kusanyiko, ambamo walikuwamo wanaume, wanawake na watu wote walioweza kufahamu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Ezra, kuhani, akaileta Torati mbele ya mkutano mzima, wanaume na wanawake, na wote walioweza kusikia na kufahamu, siku ya kwanza ya mwezi wa saba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ezra, ambaye alikuwa kuhani, akaenda na kukileta kitabu cha sheria ya Mose mbele ya mkutano mzima, wanaume kwa wanawake na yeyote aliyeweza kuielewa hiyo sheria aliposikia. Siku hiyo ilikuwa ni siku ya kwanza ya mwezi wa saba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtambikaji Ezera akayaleta Maonyo, akayaweka mbele ya huo mkutano, kwani walikuja waume kwa wake na wote walioweza kusikia na kutambua maana, ikawa siku ya kwanza ya mwezi wa saba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Ezra, kuhani, akaileta torati mbele ya kusanyiko, la wanaume na wanawake, na wote walioweza kusikia na kufahamu, siku ya kwanza na mwezi wa saba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ezra, ambaye alikuwa kuhani, akaenda na kuleta kitabu cha Sheria ya Musa mbele ya mukutano wote, wanaume na wanawake na yeyote aliyeweza kuelewa ile sheria. Siku hiyo ilikuwa ni siku ya kwanza ya mwezi wa saba.